Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wasaidizi wa Samia matumbo joto, kupanguliwa wakati wowote
Habari za Siasa

Wasaidizi wa Samia matumbo joto, kupanguliwa wakati wowote

Spread the love

RAIS wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amesema amekusudia kufanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi wa Serikali ili kuachana na viongozi ambao wanashindwa kuendana na kasi yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea). 

Dk Samia amesema hayo leo tarehe 8 Disemba 2022 katika Mkutano wa 10 wa chama hicho ambao leo umefikia tamatu mkoani Dodoma.

Amesema kuwa bado wanasafari ya miaka mitatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2025, ili wananchi wawe mashuhuda wa yanayofanywa.

“Kubwa zaidi tunapokwenda kwa wananchi, ni wananchi wenyewe wanayosema serikali waliyofanya kwao, tofauti na utamaduni tuliokuwa nao nyuma, kwamba tunapokwenda kwa wananchi serikali ndio tunawaambiwa tumewafanyia, wakati mwingine wanashangaa hiki kimefanyika wapi,” amesema Dk. Samia.

Amesema mabadiliko hayo yatatoa nafasi kwa wananchi kuona na kutoa tathmini ya yaliyofanyika na wenyewe kuwa mashuhuda wa kila kinachofanyika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

Habari za Siasa

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu...

error: Content is protected !!