Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kikwete amtaka Samia kuwa mkali ‘usivumilie upuuzi’
Habari za SiasaTangulizi

Kikwete amtaka Samia kuwa mkali ‘usivumilie upuuzi’

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete
Spread the love

RAIS mstaafu Dk. Jakaya Kikwete ameushauri uongozi mpya wa CCM unaongozwa na Mwenyekiti Dk Samia Suluhu Hassan kuwa wakali na kutovumilia maneno yanayokigawa chama hicho na badala yake watu wanaotoa kauli hizo waitwe kwenye maadili na kuonywa.

Pia amesema hamuoni Mwana CCM atakayechukua fomu kumpinga Samia katika uchaguzi mkuu mwaka 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Kikwete ametoa kauli hiyo jana tarehe 8 Disemba 2022 wakati akihutubia mkutano wa 10 wa chama hicho uliofikia tamati jiji Dodoma.

Amesema ni ukweli uliodhahiri kwamba hapa Tanzania hakuna mwanasiasa maarufu kumshinda Rais Samia.

“Usisumbuliwe na maneno hayo. Ni waombe ndugu zangu acheni uongo. Ukiangalia huko mitandaoni kuna maneno mengi ya uongo, ni upuuzi tu… tuache hii tabia ndiyo inakigawa Chama chetu.

“Mnawafanya viongozi wetu wapate stress (jakamoyo) tu. Mkiwasikia watu wanasema maneno waiteni kwenye maadili na kama hana maelezo aambiwe aache uongo.

“Hii ndio njia pekee itakayo ondoa uchimbi. Chama chetu ni kikubwa sana hakistahili kuvumilia upuuzi kama huo. Mkiuvumilia Chama hiki kitavurugika kwa maslahi ya wapuuzi. Naomba muwe wakali,” amesema Dk. Kikwete.

3 Comments

  • Kuna ubaya gani kama mwana CCM anafiiria au anaota au anadokeza kuwa angependa naye kugombea urais mwaka 2025? Si haki yake ya kikatiba? Kwanini aitwe mpuuzi au msaliti? Katiba gani imesema Mama Samia hwezi kuwa na mgombea mwenzake? Acheni udikteta katika chama

  • Kama kuna upuuzi mkubwa ni ule wa Mzee Makamba kusema kuwa Kikwete hakufa kwa sababu ni mtu mzuri
    Kikwete badala ya kukanusha ameonekana akiche tu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa matokeo ya mtihani kidato cha nne 2022

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza matokeo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

HabariTangulizi

Bakwata wamkangaa Sheikh wa Dar es Salaam

Spread the love  BARAZA la Ulamaa, limefutilia mbali uamuzi wa “kuvunja ndoa,”...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

error: Content is protected !!