Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Exim yatoa msaada wa majaketi ya viakisi mwanga kwa bodaboda Mwanza
Habari Mchanganyiko

Exim yatoa msaada wa majaketi ya viakisi mwanga kwa bodaboda Mwanza

Spread the love

BENKI ya Exim tawi la Mwanza imekabidhi msaada wa majaketi yenye viakisi mwanga (Reflector Jackets) kwa madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wa mkoani humo ikiwa ni sehemu ya jitihada ya benki hiyo katika kukabiliana na ajali za barabarani zinazotokea mkoani humo

Meneja wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Mwanza, Edwin Polle (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa majaketi yenye viakisi mwanga (Reflector Jackets) kwa Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mwanza, ASP. Sunday Ibrahim kwa ajili ya madereva wa pikipiki wa mkoa huo ikiwa ni sehemu ya jitihada ya benki hiyo katika kukabiliana na ajali za barabarani mwishoni mwa mwaka. Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja Mahusiano wa benki hiyo mkoa wa Mwanza, Sarah Tito.  Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye tawi la benki hiyo mkoani Mwanza jana.

hususani nyakati za usiku. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).


Hafla ya makabidhiano ya majaketi hayo ilifanyika kwenye tawi la benki hiyo mkoani humo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo maofisa wa benki hiyo wakiongozwa na Meneja wa Benki hiyo tawi la Mwanza, Edwin Polle, Meneja Mahusiano wa benki hiyo mkoa wa Mwanza, Sarah Tito, wawakilishi kutoka jeshi la Polisi, kikosi cha Usalama Barabarani wakiongozwa na Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Mwanza, ASP. Sunday Ibrahim pamoja na wawakilishi wa madereva wa pikipiki mkoa huo.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mwanza, ASP. Sunday Ibrahim (katikati) akikabidhi sehemu ya msaada wa majaketi yenye viakisi mwanga (Reflector Jackets) kwa ajili ya madereva wa pikipiki wa mkoa huo yaliyotolewa na Benki ya Exim tawi la Mwanza ikiwa ni sehemu ya jitihada ya benki hiyo katika kukabiliana na ajali za barabarani mwishoni mwa mwaka. Wanaoshuhudia ni pamoja Meneja wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Mwanza, Edwin Polle (kushoto). Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye tawi la benki hiyo mkoani Mwanza jana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!