Saturday , 27 April 2024
Home Politics Mjadala deni ya Taifa: Chadema wataka mikataba ya mikopo iweke wazi
PoliticsTangulizi

Mjadala deni ya Taifa: Chadema wataka mikataba ya mikopo iweke wazi

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka Serikali iweke wazi mikataba ya mikopo inayokopa katika taasisi za kimataifa, ili kujua masharti yake na sababu za ongezeko la deni la taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa jana Jumatano, tarehe 15 Desemba 2022 na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, akizungumza na Bunge la Wananchi lililoanzishwa na chama hicho kwa ajili ya kutoa nafasi kwa waliokuwa wagombea wake ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, kuwasemea wananchi wa maeneo yao.

Mnyika ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho mjadala kuhusu ongezeko la deni la taifa, umeshika kasi.

“Hatari kubwa zaidi ni juu ya nchi yetu na rasilimali zake sababu kwa bahati mbaya mikataba ya mikopo inayokopwa kwa wingi mkubwa haiwekwi hadharani. Tulivyokuwa bungeni tulikuwa na wasaa wa kujua hii mikataba. Iko mikataba ambayo dhamana ya mkoopo iliywekwa ni rasilimali za nchi. Tumeshaanza kuona jirani zetu baadhi ya rasilimali zao zinapokonywa kwa sababu ya madeni makubwa,” alidai Mnyika.

Mnyika amelitaka Bunge la Wananchi la Chadema, kupaza sauti zao kuhoji fedha za mikopo hiyo “sisi tuko kimya kama taifa, hatudai mikataba kuwa wazi. Hatudai kuulizia hizi pesa zilizokopwa zimetumika kwenye nini chenye tija na kiasi gani ambayo inarudisha ile pesa bila kulazimika kuingia kwenye hatari ya mbele kama taifa,”

“Hatuyajadili haya sababu bunge haliyajadili, sasa ninyi kwa niaba ya wananchi muayajadili hayo na mtoe muelekeo mbadala wa kuishauri Serikali.”

Katibu Mkuu huyo wa Chadema, alidai ongezeko la deni hilo ni hatari kwa kuwa itafikia mahali Serikali itashindwa kutekeleza miradi mipya ya maendeleo kutokana na kutenga fedha nyingi kwa ajili ya kulipa madeni.

“Leo tunazungumza deni la taifa limekuwa kwa kipindi cha miaka miwili na utawala mpya umeingia, deni lilikuwa linakuwa kwa kasi wakati wa Hayati John Magufuli, lakini kasi hiyo imeongezeka wakati wa utawala wa Rais wa sasa. Deni limekuwa kutoka Sh. 64 trilioni, leo tunazungumza limefikia Sh. 91 trilioni. Hii ni kengele ya hatari sana,”alidai Mnyika.

Mnyika alidai “ni ishara ya hatari kubwa sababu Chadema tutakapoingia madarakani tutakuta Serikali yenye madeni kiasi kwamba huwezi kuja na mipango mipya kwa sababu kila ukikusanya kodi za wananchi zinatumbukia katika kapu la kulipa madeni kila mwezi.”

Kufuatia mjadala wa onegezeko la deni la taifa kushika kasi, Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, ilitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo ikisema deni hilo limeongezeka kutokana na sekta binafsi kukopa kiasi cha Sh. 20 trilioni.

Dk. Mwigulu alisema kuwa, deni la sekta binafsi likijumlisha na deni la Serikali la Sh. 71.2 trilioni , linafanya deni la taifa kuwa Sh. 91 trilioni.

Waziri huyo wa fedha, alisema mikopo inayokopwa na Serikali ni ya masharti na nafuu, ambapo fedha hizo hutumika katika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ili kuimarisha uchumi na kwamba deni hilo ni himilivu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!