Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko EWURA yatangaza bei mpya za mafuta
Habari Mchanganyiko

EWURA yatangaza bei mpya za mafuta

Spread the love

 

MAMLAMKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya za mafuta. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Bei hizo zimetangazwa leo Jumanne, tarehe 1 Machi 2022 na Meneja Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo, akizungumza na wanahabari jijini Dodoma, baada ya Serikali ya Tanzania, kusimamisha tozo ya Sh. 100 kwa kila lita moja ya mafuta.

Kwa miezi mitatu mfululizo (Machi hadi Mei, 2022), ili kupunguza makali ya kupanda kwa bei ya nishati hiyo katika soko la dunia, kulikosababishwa na vita kati ya Urusi na Ukraine.

“Kimsingi ukizingatia toleo lililopita, kumekuwa na ongezeko kidogo. Lakini hilo ongezeko limemezwa na hatua ya Serikali chini ya Waziri wa Nishati, January Makamba, kuchukua hatua za kuahirisha ukusanyaji wa tozo kwenye bidhaa za mafuta,” amesema Kaguo.

Kaguo amesema “imesadiaia kidogo kupunguza mauamivu ya bei ya mafuta kwa maana kwamba bei mnazoziona kuna upungufu wa Sh. 100 kwa kila bei.”

Meneja Mawasiliano huyo wa Ewura, amesema kuanzisha kesho Jumatano, tarehe 2 Machi 2022, bei ya lita moja ya mafuta ya Petroli yanayoshushwa katika Bandari ya Dar es Salaam, itakuwa Sh. 2,540, Dizeli (Sh. 2,403) na mafuta ya taa (Sh. 2,208).

“Kama Serikali kupitia Waziri Makamba isingeahirisha utozwaji wa kodi hizi, bei ya Dar es Salaam ingekuwa Sh 2,640 kwa Petroli, Sh. 2,503 kwa Dizeli na Sh. 2,308 kwa mafuta ya taa,” amesema Kaguo.

Kaguo ametaja bei ya mafuta yaliyoshushwa katika Bandari ya Tanga, ambapo lita moja ya Petroli itakuwa Sh. 2,563, Dizeli (Sh. 2,484) na ya taa (Sh. 2,254).

Kwa upande wa mafuta yaliyoshushwa katika Bandari ya Mtwara, Kaguo amesema lita moja ya Petroli itauzwa kwa Sh. 2,577, Dizeli (Sh. 2,530) na mafuta ya taa (Sh. 2,280).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!