Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Dube kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu
Michezo

Dube kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu

Prince Dube
Spread the love

MSHAMBULIAJI wa Azam FC na timu ya Taifa ya Zimbabwe, Price Dube ataondoka nchini Jumapili ya tarehe 29 Novemba, 2020, kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu mara baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga uliochezwa jana. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo ambao ulimalizika kwa Azam FC kupoteza kwa bao 1-0, kwenye dakika 48 likifungwa na Deus Kaseke na kuifanya Yanga kuibuka na pointi tatu na kukaa juu kwenye msimamo wa Ligi.

Dube aliumia dakika ya 15 ya mchezo kwa kuvunjika mfupa wa mbele wa mkono wakati alipoanguka vibaya wakati akiwania mpira wa juu na beki wa kati ya Yanga, Bakari Mwamnyeto na kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Richard Djodi.

Taarifa kutoka ndani ya Azam FC imeeleza kuwa mara baada ya kuumia Dube alipatiwa huduma ya kwanza na baadae kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Dube ataondoka na Shirika la ndege la Kenya na atapatiwa matibabu kwenye hospitali ya Vincent Pallotti iliyopo kwenye mji wa Cape Town, Afrika Kusini chini ya daktari bingwa wa mifupa Robert Nicolas.

Mshambuliaji huyo alijiunga na timu hiyo wakati wa dirisha kubwa la usajili akitokea klabu ya Highlanders FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zimbabwe.

Mpaka sasa Dube ameshapachika jumla ya mabao sita na kuwa kinara wa mabao ndani ya klabu yake, huku akiwa nyuma kwa bao moja na kinara wa mabao wa Ligi Kuu, John Bocco mwenye mabao saba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!