RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitahakikisha mgombea wake Dk. Hussein Mwinyi anashinda urais visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).
“Wana CCM wanaoipenda Zanzibar wanasubiri wakati ufike wamchague Dk. Mwinyi, sisi tuliopo Zanzibar tutahakikisha Dk. Mwinyi anashinda,” amesema Dk. Shein leo tarehe 29 Agosti 2020 kwenye uzinduzi wa kampeni ya chama hicho Dodoma.
Amesema, Dk. Hussein anafahamika ndani na nje ya nchi pia ni maarufu ndani na nje ya nchi, na kwamba ana sifa zote za kuwa rais wa visiwa hivyo.
“Dk. Mwinyi ana uwezo mkubwa sana, ni msomi aliyebobea, yeye ni daktari bingwa na anayeheshimika ndani ya nchi na nje ya nchi. Sifa hizo ndio zilizomfanya CCM imchaguea, Dk Mwinyi ni mzalendo sana, kazi zote alizokabidhiwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezifanya kwa ufanisi mkubwa.

“Kwenye Wizara ya Ulinzi, Naibu Waziri wa Aya, Waziri wa Afya afya naibu kote huko kafanya kwa ufanisi mkubwa. Mimi naamini kama nyinyi wengi mnavyoamini Dk. Mwinyi atatuvusha Zanzibar,” amesema Dk. Shein.
Kiongozi huyo wa Zanzibar anayemaliza muda wake amesema, wakati huu wanapozindua kampeni, wana CCM wanapaswa kujua kwamba kazi ya kupeleka mbele gurudumu la maisha haiwezi kukamilika bila kuchagua wabunge, madiwani na wawakilishi kutoka CCM.
“Nakuombeni sana leo tunapozindua kampeni na ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 – 2025, sote tuwachague viongozi wetu wa CCM. Wawili hao hawawezi kufanya kazi peke yao, lazima tuwachague wabunge, wawakilishi na madiwani wote wa CCM, tusiache nafasi hata moja wazi,” amesema.
Kwenye hadhara hivyo, Dk. Mwinyi amesema Zanzibar wako tayari kuchagua viongozi wote wa CCM, Rais wa Tanzania Bara, wabunge na wawakilishi.
“Kule tunasubiri wakati wa uchaguzi. Kazi yetu mwaka huu imekuwa nyepesi kutoka na Dk shein kutekeleza vizuri sana ilani ya chama. Huku bara mambo yanaonekana wazi, Zanzibar mambo yametekelezwa sana, hivyo inatupa kila sababu wagombea wa mwaka huu kupita kwa kishindo na hilo hatuna shaka nalo,” amesema.
Leave a comment