Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Gwajima alia na uhaba wa maafisa ustawi wa jamii
Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima alia na uhaba wa maafisa ustawi wa jamii

Spread the love

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima, amesema wizara yake ina uhaba wa maafisa maendeleo ya jamii zaidi ya 2,000 ikiwa ni sawa na upungufu wa asilimia 43 kati ya 5,296 wanaohitajika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Dk. Gwajima ametaja upungufu huo leo Jumatatu, tarehe 30 Mei 2022, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, ambapo ameliomba Bunge lipitishe bajeti ya Sh. bilioni 43.40.

“Pamoja na juhudi zote za ushirikishaji jamii zinazofanywa na maafisa maendeleo ya jamii nchini, bado tunakabiliana na changamoto ya uhaba wa maafisa hao. Jumla ya maafisa 5,296 wanahitajika nchini, hadi Aprili 2022, maaafisa waliopo katika ngazi ya mkoa, halmashauri na kata ni 3,014 ambapo upungufu ni 2,282,” amesema Dk. Gwajima.

Kufuatia upungufu huo, Dk. Gwajima amesema wizara yake itaendelea kuwasiliana na Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, pamoja na Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ili kutafuta namna ya kutatua changamoto hiyo.

Aidha, Dk. Gwajima ametoa wito kwa wadau wa maendeleo yakiwemo Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kutoa ajira za muda kwa maafisa maendeleo ya jamii hususan katika ngazi ya kata ambako kuna upungufu mkubwa.

“Nitoe rai kwa wadau wa maendeleo yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali, kutoa ajira za muda kwa maafisa maendeleo ya jamii hususan katika ngazi ya kata, ambapo kuna upungufu mkubwa ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa afua za kutatua changamoto zinazoikabili jamii yetu,” amesema Dk. Gwajima na kuongeza:

“ Pia, wizara inatoa wito kwa wote wenye taaluma ya maendeleo ya jamii, ambao wapo katika jamii baada ya kustaafu wajitokeze ili kuendelea kutoa mchango wao kwenye jamii. Kama ambavyo taaluma zingine zimekuwa zikifanya. Lengo ni kila mzalendo mwenye nafasi na nia ya kuchangia maendeleo ya jamii apewe nafasi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!