September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ekari 140 zatengwa ujenzi soko la kimataifa mpakani mwa Tanzania, Kenya

Spread the love

SERIKALI kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Moshi imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 140 katika eneo la Lokolova kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Kimataifa la mpakani mwa Tanzania na Kenya. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 30 Mei, 2021 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Vunjo, Dk. Charles Kimei (CCM).

Dk. Kimei ameuliza; Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa soko la Kimataifa katika eneo la Lokolova mpakani mwa Tanzania na Kenya?

Pia amehoji ni lini Serikali itaanza kuboresha mazingira ya masoko ya vijijini yanayotumiwa zaidi na wanawake kama ilivyoboresha masoko ya mijini kwa kuweka mapaa katika maeneo hayo yanayotumiwa na wamachinga?

Aidha, Naibu Waziri alijibu tayari serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Moshi imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 140 katika eneo la Lokolova kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Kimataifa la mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Amesema hatua inayofuata ni kupata hati miliki ya eneo hilo na hatimaye kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Soko hilo.

Kuhusu uezekaji wa mapaa katika masoko hayo ya vijijini, Kigahe amesema masoko hayo yanahudumiwa na Halmashauri kupitia TAMISEMI, hivyo ametoa wito kwa halmashauri husika kutenga fedha kwa ajili ya kuezeka mapaa ya masoko hayo ili bidhaa za akina mama wafanyabiashara zisiharibike.

error: Content is protected !!