Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Biteko: Msitishwe na wapiga dili migodini
Habari Mchanganyiko

Dk. Biteko: Msitishwe na wapiga dili migodini

Waziri wa Madini, Dotto Biteko
Spread the love

 

WAZIRI wa Madini, Dk. Dotto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa dhahabu wasitishwe na vyeo vya watu wanaofika katika maeneo yao ya migodi kwa kuwa wengi ni wapiga dili. Anaripoti Paul Kayanda, Kahama … (endelea).

Pia ametoa wito kwa wachimbaji hao kutokuwa wababaishaji katika utendaji wao wa shughuli za uchimbaji wa madini hayo.

Dk. Biteko ametoa kauli hiyo juzi tarehe 27 Disemba, 2021 akizungumza na Vikundi vya Wachimbaji wadogo wanawake katika Mkoa wa Shinyanga (TAWOMA), katika kijiji cha Wisolele Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.

Dk. Biteko alipita katika Kijiji hicho kwa lengo la kusikiliza changamoto za Wachimbaji wadogo wakati akielekea katika mgodi mkubwa wa Bulyanghulu unaomilikiwa na kampuni ya Barrick.

Amewataka wachimbaji hao wasitishwe na vyeo vya watu hao kwani lengo lao ni kujipatia fedha bila jasho.

Dk. Biteko alisema anazo taarifa kwa baadhi ya watu kutumia vyeo vyao kwenda katika maeneo ya Uchimbaji kuwatishia ili kujipatia fedha, jambo ambalo alilikemea na kutotaka lisijirudie huku akiwataka wahusika wajitathmini na kutogeuza maeneo ya uchimbaji kuwa sehemu ya kwenda kupiga dili.

Akizungumzia kuhusu ushiriki wa wanawake katika shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu alisema kuwa Tanzania kuna chama cha akinamama wanaojishughulisha na uchimbaji wa Madini kinaitwa TAOMA, na kuongeza kuwa wanawake kupitia chama chao wamepewa nafasi kubwa

“Na hata nilipokuja Kahama niliwaambia maafisa wangu kuwa ule utaratibu wa watu kusimamia Rush yaani maeneo yenye mlipuko wa dhahabu basi na wanawake wapewe nafasi ya kusimamia hiyo migodi kupitia vikundi kwani wanaweza. Tunachotaka kama serikali na wanawake washiriki shughuli za uchimbaji,” alisema Dk.Biteko.

Biteko alisema kuwa Wanawake ni waaminifu kwanza hawataweza kutorosha dhahabu kama ilivyo desturi ya wanaume na kuongeza kuwa tangu sewrikali ianze kukamata watu wanaotorosha dhahabu hawajawahi kukama mwanamke ambaye anajihusisha na suala hilo.

Naye Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa Dahahabu katika Mkoa wa Kimadini Kahama(SHIREMA), Joseph Andrea Nalimi alisema kwa sasa wachimbaji wadogo ni waelewa na wakipata dhahabu hupeleka katika masoko yaliyoanzishwa na serikali hivyo kufuatia uwepo wa masoko kesi nyingi za utoroshaji zipepungua kwa kiasi kikubwa.

“Wito wangu kwa wachimbaji wa dhahabu liheshimiwe, waendelee kufuata utaratibu unaoelekezwa na serikali ukilinganisha masoko serikali imetusogezea mpaka mlangoni, naamini iwe hivyo kwa kuwa sisi wachimbaji wadogo tulisha kuwa waelewa,” alisema.

Awali vikundi hivyo vya wanawake wanaojihusisha na shughuli za Uchimbaji wa Madini aina ya dhahabu katika Mkoa wa Shinyanga vilimuomba Dk. Biteko viweze kusimamia maeneo ya mfumuko wa Dhahabu (RUSH).

Mwenyekiti TAWOMA, Semen John alimshukuru Biteko pamoja na wizara yake kwa kukumbuka kuwajali wanawake kwa kuwapatia leseni nyingi za uchimbaji wa dhahabu katika mkoa wa Shinyanga kwani nao wanajiona ni watu kama walivyo wengine.

“Nampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kitendo cha kutujali sisi wanawake mpaka na sisi tunamiliki leseni za uchimbaji wa dhahabu katika Mkoa wetu wa Shinyanga, tumepata leseni za uchimbaji huko mgodi wa Mwime Kahama, kikundi cha Uvumilivu kimepata leseni kwa hiyo Waziri tunaomba uendelee kututafutia maeneo mengine yenye Madini wanawake tuchimbe,” alisema.

Nao wachimbaji wengine wa dhahabu katika Kijiji hicho Nestory Masele alitumia fursa hiyo kumuomba Waziri wapunguziwe utitiri wa tozo na mikopo kwa wale ambao wanaweza kukopesheka.

“Mheshimiwa Waziri mwenye changamoto kubwa inayotukabili wachimbaji ni mitaji hapa kwenye eneo letu la uchimbaji hatuoni faida kwa kuwa tunatumia gharama kubwa za uendeshaji kwenye maduara ikiwemo tozo nyingi za kodi ya serikali hivyo serikali ione umuhimu wa kuwezesha suala la mikopo kwa wanaostahili kupewa ili tuweze kumudu gharama za uendeshaji vinginevyo tutazikimbia Dhahabu,” alisema mchimbaji Masele.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!