November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Djuma Shaban hati hati kuikosa Dodoma Jiji

Spread the love

 

MLINZI wa kulia wa klabu ya Yanga Raia wa Jamhuri ya Congo, Djuma Shaban yupo hati hati kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Dodoma Jiji kutokana na kupata majeruhi kwenye mchezo uliopita dhidi ya Biashara United. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utapigwa siku ya kesho tarehe 31 Desemba 2021, majira ya saa 1 kamili usiku kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akithibitisha taarifa za majeruhi ya mchezaji huyo kocha msaidizi wa klabu ya Yanga Cedric Kaze hii leo tarehe 30 Desemba 2021 kwenye mkutano wa waandishi wa habari alifunguka kuwa huwenda wakakosa huduma ya Djuma Shabani kwenye mchezo huo dhidi ya Dodoma Jiji.

“Kwenye mchezo dhidi ya Dodoma tutawakosa Djigui Diara ambaye ameenda Afcon na pia Djuma Shaban yupo kwenye hati hati ya kukosa mchezo huo kutokana na kupata majeruhi kwenye mchezo dhidi ya Biashara United.” Alisema Kaze

Katika mchezo huo dhidi ya Biashara United Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, huku mlinzi huyo wa kulia akitoa pasi moja ya bao (Assist) ambalo lilifungwa na Fiston Mayele kwa njia ya kubinuka (Acrobatic).

Wachezaji hao wote wawili ambao wanaukosa mchezo huo, wamesajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili na kuonesha kiwango kikubwa katika michezo mbalimbali ya kimashindano waliocheza.

Pamoja na Djuma Shaban kuumia lakini pia bado amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Congo sambamba na Yanick Bangala na Mukoko Tonombe.

Wachezaji hao wameitwa kwenye kikosi hiko kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki katika kujiweka sawa kwa ajili ya michezo ya kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar 2022.

error: Content is protected !!