July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Djuma Shabani rasmi atua Yanga

Djuma Shaban akisaini mkataba wa kuitumikia Yanga

Spread the love

 

ALIYEKUWA mlinzi wa kulia wa klabu ya AS Vita ya nchini DR Congo, Djuma Shaban rasmi kukipiga ndani ya Yanga, kwenye msimu ujao kufuatia kuonekana kwa picha zake akisaini mkataba huo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Awali zililipotiwa taarifa za taarifa za kuwa Yanga wamemalizana na mchezaji huyo, kufuatia kuonekana nchini Congo kwa Mhandisi Hersi Said ambaye ni mkurugezni wa uwekezaji wa kampuni ya GSM, ambao wanasimamia masuala yote ya usajili ndani ya klabu ya Yanga.

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, ilionesha picha za mchezaji huyo akisaini mktaba huo, mbele ya Hersi huku akiwa amevalia jezi ya Yanga.

Klabu hiyo imeanza usajili wake mapema, katika kujiweka sawa na msimu ujao wa mashindao kutokana na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, anajiunga na Yanga, baada ya kuhudumu ndani ya AS Vita ndani ya misimu minne toka mwaka 2017.

Licha ya kuonekana kwa picha hizo, lakini mpaka sasa uongozi wa Yanga, haujathibitisha chochote juu ya usajili huo.

error: Content is protected !!