Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande
Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the love

 

DEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya Msingi ya Ghati Memorial, iliyouawa watu tisa wakiwemo wanafunzi nane, Lukuman Hemed, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya nya Arusha, akikabiliwa na mashtaka nane ikiwemo la kuuwa bila kukusidia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Hemed amefikishwa mahakamani leo tarehe 17 Aprili 2024 na kusomewa mashtaka hayo na mawakili wa serikali, Yunsi Makala na Amina Kiango, mbele ya Haki Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Sheila Manento.

Katika kesi hiyo, Hemed anadaiwa kutenda makosa hayo tarehe 12 Aprili 2024, majira ya saa 12 asubuhi baada ya kufanya uzembe uliopelekea basi alilokuwa anaendesha likiwa na wanafunzi 13, kusukumwa na maji ya mafuriko na kutumbukia katika korongo la maji.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 30 Aprili 2024,kwa ajili ya kutajwa, baada ya mawakili wa serikali kudai upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Manento alisema dhamana ya mtuhumiwa iko wazi, lakini Hemed aliomba asipewe dhamana badala yake apelekwe mahabusu gerezani akihofiwa hasira za wananchi kufuatia vifo na madhara yaliyojitokeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari Mchanganyiko

Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba

Spread the love MKUU wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

error: Content is protected !!