Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa DC, Mbunge Chadema waungana kupinga mradi wa maji
Habari za Siasa

DC, Mbunge Chadema waungana kupinga mradi wa maji

Kunti Yusuph Majala Mbunge wa Viti Maalum Kunti Yusufu Majala (Chadema)
Spread the love

SAMSON Odunga Mkuu wa Wilaya ya Chemba na Mbunge wa Viti Maalum Kunti Yusufu Majala (Chadema), wamewataka wananchi wa wilaya hiyo kuukataa mradi wa maji wa Ntomoko kwa madai ya uwepo wa viashiria vya rushwa, anaandika Dany Tibason.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Songoro, kijiji cha Hamai wilayani Chemba wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, Mbunge wa viti maalum alisema hakuna sababu yoyote ya wananchi kukubaliana na mradi huo kwani hauna faida kwa wananchi hao.

“Watu wa Hamai mnataabika sana, maji ya uhakika hakuna. Tumekuwa tukiambiwa kuwa kuna mradi wa maji wa Ntomoko, mradi huo hautekelezeki kwani mpaka sasa ni zaidi ya miaka 7 mradi huo hautoi maji na wananchi wanaendelea kutaabika.

“Nawaomba sana wananchi tusikubaliane na mradi huo, tuukatae na tutafute mradi mbadala utakaotekelezeka kwa faida ya wananchi.”

Kwa upande wake Samson Odunda, mkuu wa wilaya hiyo amesema anaunga mkono ushauri wa Mbunge Kunti Yusufu, wa kuukataa mradi huo kwani hautekelezeki.

“Kuna wajanja wachache wamekula fedha za mradi huu na kusababisha mradi kusuasua tangu ulipoanza kutekelezwa Machi 2014 kwa thanani ya Sh. 2.8 na ulitakiwa kukabidhiwa rasmi Septemba 2016.

“Mpaka sasa mradi umeshatumia Sh. 2 bilioni bila mafanikio yoyote na ulitakiwa kuhudumia vijiji kumi katika wilaya za Kondoa na Chemba ambavyo ni; Makirinya, Hamai, Chiruku, Songolo, Lusangi, Kirere,   Chang’ombe, Kinkima, Madaha, Jinjo na Jangalo,” amesema.

Mkuu huyo wa wilaya amesema tayari ameagiza Taasisisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kufanya uchunguzi ili kubaini ubadhirifu uliokwamisha mradi huo.

“Nimepokea ripoti ya PPRA inayoonesha madudu makubwa ambayo yanaonesha wazi kuwa mradi umekwama kutokana na kuwepo kwa vitendo vya rushwa,” amesisitiza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!