Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni
Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love

 

MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewataka wazazi kupeleka chakula shuleni, ili watoto wasiwe watoro, hali ambayo itaongeza ufaulu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

DC Mgeni ametoa maelekezo hayo wakati akiwa kwenye ziara katika Kata ya Ruvu, Tarafa ya Same ambapo ameweza kukagua mradi wa ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Moipo ambao umegharimu shilingi milion 126 na mradi wa kituo cha Afya cha Tarafa.

Pia DC Kasilda  amefanya mkutano wa hadhara katika kata hiyo ya Ruvu ambapo amewasisitiza wazazi kuhakikisha wanapeleka chakula cha mchana ili watoto waweze kupata chakula wakati wa kiwa shuleni lengo ni kuondoa utoro, ili kupata ufaulu mzuri kwa watoto.

Mkuu huyo wa wilaya amemwelekeza mhandisi kuhakikisha fedha za nyongeza kiasi cha shilingi milioni 30 za ujenzi wa bweni la Sekondari Moipo zinakamilisha ujenzi huo ifikapo Aprili 08, 2023.

Aidha, ameelekeza wananchi kuepuka desturi ziziso za kiafrika hususani za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ubakaji na ulawiti  na kuhakikisha wanakemea vitendo hivyo vinavyochochea maadili kuporomoka na kurudisha maendeleo nyuma.

DC Kaslida  amewataka wananchi kusimamia miradi yote inayotekelezwa na serikali ili kuweza kuilinda na waendelee kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vya rushwa ndani ya mradi

Kwa upande mwingine, Kaslida amewataka   wakulima na wafugaji kuendelea kuheshimiana kwa kutoingiza mifungo ndani ya mashamba na wakulima kutolima maeneo ya mifungo kwa kufanya hivyo migogoro ya wakulima na wafugaji itapotea kabisa.

2 Comments

  • Wapambania haki za Binadamu wamebuni Mbinu za Mwanamke kupata SIFA ZINAZOSTAHIZI KWA KUMWEKEA VIKWAZON VYA KILA MTU ANATAKIWA KUMUONA MWANAE ALIYEMZAA (MZEE/kabila ANATAKA URAIS KULE ULIKOENDA KUONA). MHE ULIKOOA KULE KUNA MTU ANATAKIWA KUGAWA NCHI YA TANZANIA KILA MKOA UWE NCHI.. … MHE. KULE ULIKOOA KUNA MTU ANAMAWAZO YA NYERERE TUMECHOKA

    KAMA UNA MATOTO WA KIKE UNAJUA FURSA ULIONAYO KAMA MZAZI

    KAMA UNA MTOTO WA KIUME UNAJUA FURSA ULIYONAYO USIMSAHAU BASH YUPO KULE

  • Wapambania haki za Binadamu wamebuni Mbinu za Mwanamke kupata SIFA ZINAZOSTAHIZI KWA KUMWEKEA VIKWAZON VYA KILA MTU ANATAKIWA KUMUONA MWANAE ALIYEMZAA (MZEE/kabila ANATAKA URAIS KULE ULIKOENDA KUONA). MHE ULIKOOA KULE KUNA MTU ANATAKIWA KUGAWA NCHI YA TANZANIA KILA MKOA UWE NCHI.. … MHE. KULE ULIKOOA KUNA MTU ANAMAWAZO YA NYERERE TUMECHOKA… MHE. KULE ULIKOOA KUNA JAMBO LETU LA KATIBA MPYA… ULIKOOA ULIPELEKA NYOTA YA WATU KUSHINDA BIKO KILA SIKU

    KAMA UNA MATOTO WA KIKE UNAJUA FURSA ULIONAYO KAMA MZAZI

    KAMA UNA MTOTO WA KIUME UNAJUA FURSA ULIYONAYO USIMSAHAU BASH YUPO KULE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!