Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo
Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia
Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Tanzania kufanya kazi kitaaluma bila uoga, upendeleo na uonevu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro …(endelea).

Kauli imetolewa leo tarehe 29 Machi 2023 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kwa niaba ya Rais Samia wakati akifungua Mkutano wa 12 wa kitaaluma wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) unaofanyika mkoani Morogoro.

” Rais Dk. Samia anawasilimia sana, ameniambia, kazungumze nao waambie wafanye kazi kitaaluma bila woga, bila upendeleo wala uonevu, haya ni maneno yake mwenyewe,” amesema Waziri Nape.

Nape amesema Rais Dk. Samia ni muumini wa haki ya kujieleza na kutoa maoni, hivyo haoni sababu ya kuminya uhuru wa Habari.

“Rais alishawahi kuniambia wakati wa mchakato ya kupitia Sheria ya Habari kuwa tuhakikishe hatuingilii haki ya watu kujieleza.

“Nasi tumekuwa tukilifanya hilo, niwaombe kwa pamoja tutafsiri maono ya Rais wetu, yeye nia na dhamira yake ni kuona uhuru wa Habari unaleta tija kwa nchi,” amesema.

Pamoja mambo mengine, Waziri Nape amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa vyombo vya Habari ingawa anaamini wapo baadhi ya watu wanakwamisha, lakini watashughulika na watu wote wanakwamisha nia njema ya Rais ya kutaka kuwe na uhuru wa kweli wa Habari.

Katika mkutano huo Waziri Nape alikabidhiwa tuzo ya heshima na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deodatus Balile ikiwa ni tuzo ya kwanza ya heshima kupewa Waziri wa Habari tangu nchi hii kupata uhuru.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!