Spread the love

JUMUIYA ya Madola Kanda ya Afrika  CPA unakusudia kujenga ofisi ya Makao Makuu ya Jumuiya hiyo pamoja na ujenzi wa hoteli ya nyota tano katika  eneo la Ndejengwa Jiji la Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea). 

Hayo yamebainishwa jana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madola ya Afrika, Muturi Jastine Muturi, ambaye pia Spika wa Bunge la Nchi ya Kenya.  

Muturi pamoja na wajumbe wengine wa Jumuiya hiyo wakiongozana na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugui walifanya ziara nchini Jijini Dodoma kwa lengo la ukaguzi wa ujenzi wa ofisi za Wizara mbalimbali katika mji wa serikali.

Pia ujumbe huo ulitembelea miradi mbalimbali kama vile, ujenzi wa stendi ya mabasi yaendayo mikoani, Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), Ukumbi wa mikutano wa Bunge pamoja Eneo kukagua eneo ambalo jumuiya hiyo itajenga ofisi hizo pamoja na kitega uchumi.

Muturi Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya ukaguzi wa Eneo hilo alisema kuwa eneo utawezesha ujenzi wa ofisi za jumuiya ya CPA na ujenzi wa vivutio pamoja na ujenzi wa Hotel ya nyotatano.

“Kwanza napenda kutoa shukrani kwa serikali ya Tanzania kwa kuweza kutoa eneo kwa ujenzi wa Ofisi ya CPA, Tulipewa eneo siku nyingi lakini leo ndo tumekuja kuliona.

“Kabla ya mwaka huu Keisha tunatrajia kuanza ujenzi wa mradi wetu na pamoja na kuwa hatujafanya tathimini ya kutosha mradi huo unaweza kugharimu kiasi cha cha dola milioni 30,” alisema Muturi.

Katika hatua nyingine, Muturi alisema kuwa amefuraishwa na miundombinu ambayo imewekwa katika eneo ambalo kuwajengwa mradi wa CPA.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe alisema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa Jiji la Dodoma unafanya kazi ya kupima Viwanja na kuweka miundombinu ambayo unaweza kumfanya mtu yoyote kuweza kujenga muda wowote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *