Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko JP DECAUX, Polisi waandaa tamasha la bodaboda 
Habari Mchanganyiko

JP DECAUX, Polisi waandaa tamasha la bodaboda 

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Kampuni ya JP DECAUX imeandaa tamasha la UNITY FESTIVAL kati ya bodaboda na askari Polisi  wa usalama barabarani litakalokuwa linatoa elimu na kuhamasisha kuzingatia sheria na usalama wa barabara. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo kwa ajali za barabarani zisizokuwa za lazima zinazosababishwa na madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda.

Mratibu wa tamasha hilo kutoka kampuni ya JP DECAUX, (jp dikox), Anna Lukolongo alisema lengo la shindano hilo ni kutoa elimu kwa bodaboda hao pamoja na kuimalisha umoja kati yao na askari Polisi jijini hapa.

Lukolongo alisema katika tamasha hilo, michezo itakayofanyika siku hiyo (Julai 20, 2019) ni pamoja na mwendashaji mwenye stamina, anayeweza kupita kwenye vikwazo mbalimbali.

Alisema mshindi katika shindano hilo, atapata zawadi ya pikipiki mpya huku washiriki wote wakipatiwa elimu ya usalama barabarani ili kupunguza ajali zilizokuwa za lazima.

Aidha Lukolongo amesema bonanza hilo litanguliwa na michezo mbalimbali,ikifuatiwa na shindano la kumpata mwendashaji bora wa bodaboda itakayosimamiwa na askari wa usalama barabarani.

Tamasha hilo limebebwa na kauli mbiu isemayo ‘SOTE NI NDUGU,’ ambapo tayari limefanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Morogoro ikiwa ni mwendelezo wa matamasha yaliyofanyika ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na China.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!