BENKI ya Diamond Trust (DTB) imepigwa faini ya kiasi cha Sh. 1 Bilioni na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kukaidi agizo la kuanzisha kituo cha taarifa hapa nchini. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BOT jana tarehe 12 Julai 2019, inaeleza kwamba, ilitoa maagizo kwa benki na taasisi zote za fedha zinazofanya shughuli zake hapa nchini, kuanzisha vituo vya taarifa ‘Data Centre’, lakini DTB haikutekeleza agizo hilo.
Sehemu ya taarifa hiyo inaeleza kuwa, BOT ilitoa barua mnamo tarehe 3 Machi 2014 na 29 February 2016 kwa ajili ya kuzielekeza benki za taasisi za fedha nchini, kuanzisha vituo hivyo kwa lengo la kuhakikisha taarifa na huduma za sekta hiyo, zinapatikana wakati wote.
“…DTB haikutekeleza maagizo, licha ya kuthibitisha kwamba imekwisha anzisha kituo cha taarifa,” inaeleza sehemu ya taarifa ya BOT .
Aidha, taarifa ya BOT imeongeza kuwa, DTB itatozwa riba ya asilimia kumi kwa kila mwezi, endapo itashindwa kulipa faini kwa muda husika.
BOT imezitaka benki na taasisi za fedha zinazofanya shughuli zake hapa nchini kuanzisha vituo vya taarifa.
Leave a comment