Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar chatoa mbinu za kukabiliana na majanga ya moto
Habari Mchanganyiko

Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar chatoa mbinu za kukabiliana na majanga ya moto

Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Dk. Lazaro Mambosasa
Spread the love

 

CHUO cha Taaluma ya Polisi Dae es salaam (DPA) kimeendelea kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali katika kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akitoa taarifa hiyo leo tarehe 30 Mei, 20223 Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Dk. Lazaro Mambosasa amesema kuwa chuo hicho kimekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa kozi mbalimbali wawapo chuoni hapo.

Ameendelea kueleza kuwa lengo la kutoa elimu hiyo ni kujenga uwezo kwa maofisa,wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi hilo na makundi mengine ya wahitaji ambapo amebainisha kuwa ni vyema kila askari kuwa na vifaa wezeshi ili kukabiliana na majanga hayo pindi yanapotokea.

Mbali na hilo Mkuu wa chuo hicho ametumia fursa hiyo kumpa pole mkufunzi wa chuoni hapo aliyepata majanga ya kuunguliwa moto nyumba yake, ambapo amebainisha kuwa kutokana na changamoto hiyo aliyoipata waliona vyema kuungana kama Jumuiya ya Chuo cha Taaluma ya Polisi kumpa Mkono wa Pole kwa kadhia aliyoipata.

Kwa upande wake Sajenti Saidi Hamad aliyepata janga hilo la kuunguliwa moto nyumba yake ameushukuru uongozi wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kwa namna walivyoguswa na tukio hilo, ameongeza kuwa nyumba yake iliyopo Zanzibar iliteketea yote kwa moto ambapo anamshukuru Mungu familia imebaki salama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

Habari Mchanganyiko

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the love  Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya...

Habari Mchanganyiko

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk....

error: Content is protected !!