Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Chumba alicholala Messi nchini Qatar kugeuzwa makumbusho
KimataifaMichezo

Chumba alicholala Messi nchini Qatar kugeuzwa makumbusho

Spread the love

 

CHUO kimoja nchini Qatar kimetangaza kuwa kina mpango wa kugeuza chumba ambacho staa wa Argentina, Lionel Messi alikuwa akitumia kama malazi yake wakati wa mashindano ya kombe la dunia kuwa sehemu ya makumbusho (makavazi). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kupitia taarifa ambazo zimechapishwa na majarida ya kimataifa, chumba hicho katika chuo kimoja ambacho timu ya taifa ya Argentina ilikuwa inalala kilikuwa kinatumiwa na Messi pamoja na rafiki wake wa muda mrefu Sergio Aguero.

Jarida la Goal.com lilinukuu chombo kimoja cha habari nchini Qatar kuwa chumba hicho sasa hakitatumiwa na mtu yeyote bali kitageuzwa kuwa makavazi madogo kama njia moja ya kumuenzi Messi.

Vitu vyote ambavyo nyota huyo wa PSG alikuwa anavitumia katika chumba hicho vitabaki chumbani humo kama maonyesho ya kifahari.

“Chumba cha mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi hakitabadilika na kitabaki kwa wageni pekee na si kwa wakazi. Mali za Messi zitakuwa urithi kwa wanafunzi na vizazi vijavyo na shahidi wa mafanikio makubwa aliyoyapata Messi wakati wa Kombe la Dunia,” alisema Hitmi al Hitmi, mkurugenzi wa mawasiliano na uhusiano wa umma katika Chuo Kikuu cha Qatar aliponukuliwa na gazeti la Qatar Al Sharq.

Argentina ilishinda Kombe lao la tatu la Dunia na la kwanza kwa Messi katika maisha yake ya soka baada ya ushindi mnono dhidi ya Ufaransa katika mchezo wa michuano ya 2022.

Meneja wa klabu yake, Christophe Galtier alikiri furaha ya kufikia hatua hiyo muhimu, lakini pia alitangaza kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 hatacheza PSG hadi katikati ya Januari.

Messi alipokea mpira wa dhahabu katika fainali ya Kombe la Dunia 2022 kwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo.

Alifunga mabao saba nyuma ya jumla ya mabao nane ya Kylian Mbappe.

Mchezaji huyo wa Ufaransa alitunukiwa kiatu cha dhahabu kwa kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.

Wiki iliyopita taarifa kutoka Argentina pia zilidai kuwa taifa hilo linatathmini hatua ya kuweka picha ya mchezaji huyo kwenye noti za nchi hiyo kama njia moja ya kumuenzi kwa umahiri wake katika ulimwengu wa soka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!