Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Upinzani DRC wawaponza mawaziri 3, wajiuzulu
Kimataifa

Upinzani DRC wawaponza mawaziri 3, wajiuzulu

Felix Tshsekedi, Rais wa DRC
Spread the love

 

MAWAZIRI watatu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao ni wanachama wa chama cha mgombea urais, Moise Katumbi wamejiuzulu leo tarehe 29 Disemba, 2022 baada ya rais wa nchi hiyo kutaka kufahamu ni nani wangemuunga mkono katika uchaguzi ujao. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Katumbi (57) – mfanyabiashara tajiri ambaye aliwahi kuongoza eneo lenye utajiri wa madini la Katanga, mapema mwezi huu alitangaza kwamba atagombea nafasi ya rais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2023.

Rais Felix Tshisekedi aliwaita leo mawaziri watano ambao ni wanachama wa chama cha Katumbi cha Ensemble pour la Republique ili kujua msimamo wao na ndipo Waziri wa mipango, waziri wa uchukuzi na naibu waziri wa afya walipowasilisha baadaye ombi lao la kujiuzulu.

Tshisekedi, ambaye aliingia madarakani Januari mwaka 2019, tayari ametangaza kuwa ana nia pia ya kugombea muhula wa pili mwaka ujao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!