Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mjukuu wa Bob Marley afariki dunia
KimataifaMichezo

Mjukuu wa Bob Marley afariki dunia

Spread the love

 

BILA shaka mwaka wa 2022 utakuwa unaeleka ukingoni huku ukiacha giza nene katika familia ya mkongwe na muasisi wa muziki aina ya Reggae, Bob Marley.

Hii ni baada ya majarida ya kimataifa hasusani kutoka Jamaica na bara Ulaya kuripoti kuwa mjukuu wa bingwa huyo wa Reggae amefariki dunia usiku wa Jumanne tarehe 27 Desemba, 2022. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Joseph Mersa Marley mwenye umri wa miaka 31 ni mjukuu wa Bob Marley ambaye pia alikuwa ni msanii na kulingana na jarida la Mail Online ambalo liliripoti kuwa Mersa Marley alipatikana akiwa amepoteza fahamu ndani ya gari lake katika jimbo moja nchini Marekani.

Msanii huyo ni mtoto wa Stephen Marley ambaye ni kijana mkubwa wa Bob Marley.

Msanii huyo – aliyefahamika kwa jina la kisanii Jo Mersa – aliripotiwa kuugua pumu maisha yake yote, na kituo cha redio cha Florida WZPP kilidai alifariki kwa shambulio la pumu.

Bob alifariki dunia kwa saratani mwaka 1981 akiwa na umri wa miaka 36, na anachukuliwa kuwa mmoja wa waanzilishi wa muziki wa reggae. Nyota huyo wa marehemu alikuwa na watoto 11 na wapenzi saba tofauti.

Mail Online waliripoti kuwa Joseph Mersa Marley alitumia miaka yake ya mapema huko Jamaika, ambapo alihudhuria Shule ya Maandalizi ya Watakatifu Peter na Paul. Kisha akahamia Florida ambapo alikuwa mwanafunzi katika Shule ya Upili ya Palmetto.

Akiwa Miami Dade College alisomea studio engineering. Mwaka 2014 alitoa EP iitwayo Comfortable na 2021 akatoka na Eternal.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!