Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Chongolo: Mabasi DART Mbagala yarejeshwe
Habari Mchanganyiko

Chongolo: Mabasi DART Mbagala yarejeshwe

Spread the love

KATIBU Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kuhakikisha mabasi ya mwendokasi yanarejeshwa katika njia ya kuelekea Mbagala ili kunusuru wananchi wa ukanda huo na adha ya usafiri. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Tarehe 27 Juni 2023 safari za mabasi hayo kati ya Gerezani hadi Mbagala rangi tatu ambayo ililenga kurahisisha huduma ya usafiri kwa watu wanaotaka kutembelea maonyesho ya sabasaba.

Hata hivyo, akizungumza katika mkutano wa CCM uliofanyika katika viwanja vya Kawe jijini Dar es Salaam, Chongolo amesema si nia ya serikali kutoa huduma kwa kipindi kifupi kifupi pekee kwa wananchi.

Ameeleza kushangazwa na Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) maarufu kwa jina la Mwendokasi kusitisha huduma hiyo baada ya maonesho ya sabasaba kumalizika.

“Wekeni utaratibu mabasi yaendelee kutoa huduma Mbagala ili wanachi waondokane na utaratibu wa kupitia madirisha, watu wanufaike na maendeleo ya huduma za miundombinu.

“Kama  mabasi ni machache, wekeni mpango haraka wa kuongeza mabasi kwa sababu Serikali imetumia mabilioni ya fedha kujenga barabara hizo,” amesema.

Amesema kazi CCM sio kusema watafanya bali pia wanataka kuona mambo yakienda kwa haraka kwa ufanisi unaotakikana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Total Energies yawekeza bilioni 17 kusambaza gesi ya kupikia

Spread the loveILI kurahisisha upatikanaji wa gesi ya kupikia kwa gharama nafuu...

error: Content is protected !!