Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yaibua maswali tata kauli ya Lugola
Habari za Siasa

Chadema yaibua maswali tata kauli ya Lugola

Spread the love

MSUGUANO kati ya Serikali ya Jamhuri na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhusu Tundu Lissu unaendelea ambapo sasa Chadema inahoji maswali matatu ‘makubwa’. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni Chadema akizungumza na wanahabari leo tarehe 14 Februari 2019 jijini Dar es Salaam ameeleza kushangazwa na wito wa Lissu kusaidia uchunguzi bila kutumia mfumo rasmi huku akiuliza maswali matatu.

Wakati Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani akisema kuwa, Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki anapaswa kurejea ili kusaidia uchunguzi wa kushambuliwa kwa risasi, Kigaila amehoji “je, serikali imempa wito rasmi?”

Lugola alieleza kuwa, madai ya Lissu kwamba siku ya tukio walinzi wa nyumba za viongozi wa serikali pamoja na kamera za ulinzi (CCTV) zilizondolewa  ni ya uongo.

Kigaila amehoji kuwa, kama eneo la tukio lilikuwa linalindwa na walinzi binafsi, vyombo vya dola vimechukua hatua gani kwa walinzi waliokuwepo pamoja na kampuni inayowasimamia?.

“Alisema eneo hilo halina ulinzi wa serikali, upo ulinzi kutoka watu binafsi. Awaambie Watanzania alikamata walinzi wangapi wa kampuni hiyo?

Mwisho amemtaka Lugola aeleze kwa nini taarifa zilizotolewa awali za uwepo wa CCTV kamera eneo la tukio zilizotolewa ndani na nje ya Bunge hazikupingwa na serikali?

Kigaila ameelekeza maswali hayo kwa Lugola na wale wanaomtaka Lissu kurejea nchini kusaidia uchunguzi ambapo wamesema, ‘kama angekuwa muhimu basi angepewa wito.’

Kigaila ameisukumia mzigo serikali kwamba, imeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kufanya uchunguzi kutokana na mbunge huyo kushambuliwa mchana kweupe.

Ofisa huyo wa Chadema amesema, kumekuwepo na msukumo na maneno yanayomtaka Lissu kurejea nchini kwa ajili ya uchunguzi bila kujali mhali yake huo, amehoji namna gani Lissu amefikiwa na kupewa wito huo?

Akiwa jijini Arusha mbele ya waandishi wa habari jana tarehe 13 Februari 2019 Lugola amesema, Lissu anapaswa kurejea nchini ili kusaidia uchanguzi wa shambulio lake.

Lissu ambaye ni mbunge wa Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, yuko nchini Ubelgiji anakopatiwa matibabu kwenye hospitali ya Chuo Kikuu cha Luvein, kufuatia kushambuwa kwa risasi nje ya nyumba yake, Area D, mjini Dodoma, tarehe 7 Septemba 2017.

Lugola alisema, Lissu anakwamisha mwenyewe uchunguzi wa tukio lake la kupigwa risasi na kwamba, “aache kuwaeleza wazungu, kwa sababu wanaopeleleza kesi siyo wao.”

Kigaila wa Chadema amesema, si kweli kwamba kutokuwepo kwa Lissu hapa nchini kunakwamisha upelelezi wa tukio hilo kwa kuwa, vyombo vya dola vina uwezo wa kuchunguza tukio pasipo mhusika kuwepo.

“Ni nani alioyeshirikiana na polisi kuchunguza tukio lake mwenyewe, kazi ya muathirika ni kwenda mahakamani kutoa ushidi ambapo anakua shahidi wa kwanza.

“Suala la Lissu liko mikononi mwa serikali linatakiwa lichunguzwe. Na kama hawawezi kwa nini wanahofu kuwaita wachunguzi wa kimataifa waje wachunguze?” amehoji Kigaila.

Tazama video kamili hapo chini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!