Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema: Tundu Lissu ana baraka zetu
Habari za Siasa

Chadema: Tundu Lissu ana baraka zetu

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kinakubaliana na ziara anazofanya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu nje ya nchi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 14 Februari 2019 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi  wa Mafunzo na Operesheni Chadema, Benson Kigaila amesema chama hicho kinakubaliana na ziara hizo.

Kigaila ameeleza kuwa, Chadema inakubaliana na ziara hizo kwa asimilia mia na ina muunga mkono kwa kuwa hakuna jambo baya ambalo Lissu analifanya kupitia ziara hiyo.

Hata hivyo, Kigaila amesema Chadema haijamtuma Lissu kufanya ziara hizo kwa ajili ya kujitangaza kama inavyodaiwa na baadhi ya watu, bali ni mkakati wake wa kuielezea dunia mambo yanayotokea hapa nchini ikiwemo kuhusu masuala ya kisiasa na tukio lake la kupigwa risasi mwishoni mwa mwaka 2017.

“Chadema inakubaliana na ziara ya Lissu kwa asilimia 100, na ni mkakati wake wa kujitangaza na wala haitangazi Chadema sababu tuna sera yetu ya mambo ya Nje. Tuna muunga mkono sababu hakuna baya analosema, anachofanya anaeleza alichotendewa,” amesema Kigaila.

Ziara za Lissu zilianzia katika bara la Ulaya ambapo alizuru katika nchi za Uingereza, Ubelgiji na kwa sasa yuko nchini Marekani, ambapo katika ziara hizo alizungumza na baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!