Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema wamvimbia Spika Ndugai
Habari za Siasa

Chadema wamvimbia Spika Ndugai

Job Ndugai, aliyekuwa Spika wa Bunge Tanzania
Spread the love

WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wameagizwa kutotii agizo la Job Ndugai, Spika wa Bunge kwamba warejeshe fedha za posho walizopewa. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema amesema, Kati Kuu ya chama hicho imetafakari na kuona kuwa, hakuna sababu ya wabunge hao kurejesha fedha hizo kama ilivyoamriwa na mahakama.

Tarehe 6 Mei 2020, Spika Ndugai aliwataka wabunge wa Chadema waliogoma kuhudhuria vikao vya bunge kwa kujiweka karantini, warejeshe fedha za posho walikopewa za Bunge.

Akisistiza agizo hilo Spika Ndugali alisema, endapo mbunge atakaidi agizo hilo, itamlazimu atakaporejea awe na cheti kinachoonesha amepima ugonjwa wa corona na majibu yake ama hatua zaidi zitachukuliwa.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 11 Mei 2020, wakati akieleza maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho, Mnyika amesema “Kamati Kuu imeagiza wabunge kutotekeleza maagizo hayo, kwa kuwa ni kinyume cha sheria.”

Amesema, Kamati Kuu kuu imejiridhisha kuwa wabunge wake wake si wezi na kwamba, fedha hizo hawajaiba hivyo hawana sababu ya kuzirejesha.

“Azimio la sita ni juu ya madai yaliyotolewa na Spika Ndugai, kwamba wabunge wa Chadema waliopewa posho za kujikimu za kuishi Dodoma ni wezi.

“Kamati imefikia uamuzi, kwamba madai haya ya spika ni ya uongo na kutoa rai kwa wabunge kutokutekeleza yale ambayo spika ameleekeza kinyume na Katiba na sheria za nchi,” amesema Mnyika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!