Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Takukuru Kinondoni yapanguliwa, uchunguzi waendelea
Habari Mchanganyiko

Takukuru Kinondoni yapanguliwa, uchunguzi waendelea

Brigedia Jenerali, John Mbungo
Spread the love

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania, Brigedia Jenerali, John Mbungo amepangua safu ya uongozi wa taasisi hiyo Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Brigedia Jenerali, Mbungo amesema amefanya uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya watendaji wake kutokutimiza wajibu wake ipasavyo.

Bosi huyo wa Takukuru amesema hayo leo Jumatatu tarehe 11 Mei 2020, wakati akijibu swali la MwanaHALISI ONLINE lililotaka kujua ni hatua zipi zimefikiwa katika uchunguzi wa baadhi ya viongozi wake wa  Mkoa wa Kinondoni na Tanga.

Kwa nyakati tofauti mwezi Machi 2020, Takukuru iliwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wake wa Kinondoni na Tanga wakiongozwa na  mabosi wa maeneo hayo kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Tarehe 20 Machi 2020, Brigedia Jenerali Bungo aliwasimamisha kazi watumishi wawili ambao ni mkuu wa taasisi hiyo mkoani Tanga, Christopher Mariba pamoja na Afisa Uchunguzi Mkuu wa Takukuru, Hilton Njauna kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakichunguzwa na taasisi hiyo.

Tarehe 26 Machi 2020, Brigedia Jenerali, Mbungo alitangaza kuwasimamisha kazi watumishi watano wa Kinondoni wakiongozwa na Mkuu wa Takukuru Kinondoni, Teddy Mjangira kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yao.

Teddy na wenzake wanatuhumiwa kufanya uchunguzi kwa mtu ambaye hakupaswa kuchunguzwa hali iliyosababisha usumbufu kwa mtu huyo.

Katika mazungumzo yake na MwanaHALISI ONLINE, Brigedia Jenerali Bungo amesema uchunguzi dhidi ya tuhuma zao unaendelea na utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Amesema kwa Mkoa wa Takukuru wa Kinondoni, “Tumewatoa maeneo yao ya kazi, Kinondoni nzima ilikuwa haijakaa vizuri. Kulikuwa na malalamiko mengi kuhusu watendaji wa Kinondoni na tumepangua safu nzima kuanzia kiongozi mkuu na tumepeleka sura mpya kabisa.”

Kuhusu uchunguzi ulipofikia mkoani Tanga, Brigedia Jenerali Bungo amesema uchunguzi umefikia hatua za mwisho akisema, “uchunghuzi uko tayari kupelekwa mahakamani, kuna mmoja tuna ushahidi wa kutosha kuweza kusimamisha mashtaka mbele.”

“Yule bosi bado tunaendelea kumchunguza, shahidi wa kumuunganisha naye alikuwa hajapatikana lakini mtumishi ambaye yeye tulimkamata kabisa na ushahidi wa rushwa huyu ndiyo tutamfikisha mahakamani,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!