Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Matangazo Carlinhos wa Yanga aisimamisha Dar, kumuona buku 5
Matangazo

Carlinhos wa Yanga aisimamisha Dar, kumuona buku 5

Spread the love

VIONGOZI wa klabu ya Yanga leo Jumanne tarehe 25 Agosti, 2020 umempokea kwa kishindo mchezaji wao mpya raia wa Angola Carlos Stenio Fernandes Guimares “Carlinhos” kwenye Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

Mchezaji huyo ambaye anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo kuanzia msimu ujao, ameingia nchini majira ya saa 7:20 na shirika la ndege la Ethiopia akitokea nchini kwao Angola.

Kilichovutia zaidi katika mapokezi hayo ni namna mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo waliojitokeza kwa wingi uwanjani hapo kutokana na kuamini uwezo wa mchezaji huyo katika kuisadia timu hiyo.

Msafara wa mchezaji huyo ulianzia Uwanja wa ndege na kupita mitaa mbalimbali katikati ya jiji la Dar es Salaam, ukiwemo mtaa wa Msimnazi ambapo ni makao makuu ya klabu ya Simba na kisha kuelekea mitaa ya Twiga na Jangwani ambapo kuna makao makuu ya klabu ya Yanga huku kukiwa na kundi kubwa la mashabiki.

Carlinhos ambaye amezaliwa 19 machi, 1995 nchini Angola amejiunga na Yanga akitokea klabu ya Interclub inayoshiriki Ligi Kuu nchini Angola, lakini pia alipitia katika klabu za Petro Luanda na Porcelana Cazengo katika maisha yake ya Soka. 

Usajili wa mchezaji huo kutaifanya idadi ya wachezaji waliosajiliwa Yanga kufika 11, kwenye dirisha kubwa la usajili linalotarajia kufungwa 31 agosti, 2020,

Wakati huohuo, Yanga wametangaza kiingilio cha maadhimisho ya Wiki ya Mwananchi iliyo kawa itemheke aamalkwenye tamasha hilo itakuwa Tsh. 5000 kwa mzunguko, Tsh. 20000 kwa upande wa VIP B na C, na Tsh. 30000 kwa VIP A

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!