TUNDU Lissu, mgombe urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mgombea mwenza wake Salum Mwalimu, wameponea kwenye ‘tundu la sindano.’ Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Lissu, Mwalimu walijikuta wakitumia zaidi ya saa saba ndani ya Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutokana na fomu zao wakati wa uhakiki kubainika kuwa na kasoro.
Kwa mujibu wa taratibu za NEC, fomu za Lissu zilikosa baadhi ya vigezo vilivyohutajika kulingana na mahitaji ya taratibu za kupitishwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Fomu za Lissu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema, zilikosa uhakiki wa taarifa za wadhamini wake 2,000 kutoka kwenye mikoa 10 kama inavyoelekeza sheria ya uchaguzi.
Badala yake Lissu na chama chake walitaka fomu hizo zihakikiwe katika ofisi za NEC, tofauti na vyama vingine ambavyo wagombea wake walihakiki fomu zao mapema na sehemu husika.
Kwa mujibu wa ratiba ya NEC ya kurudisha fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti cha urais na makamu wake, Chadema kilikuwa chama cha nne kwa wagombea wake kurudisha fomu, ambapo walipangiwa kuanza zoezi hilo saa 6:00 mchana hadi saa 6:15 mchana.
Lakini Chadema walifanikiwa kukabidhi fomu hizo saa moja kioni baada ya kukamilisha taratibu za uhakiki wa fomu. Zoezi la uhakiki wa fomu zao lilichukua takribani nusu saa ikilinganishwa na vyama vingine ambavyo vilitumia dakika 15 kulikamilisha.
Baada ya kukamilisha zoezi hilo, Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa NEC alimtangaza Lissu na Mwalimu kwamba, wameteuliwa kugombea nafasi hiyo baada ya kukidhi vigezo.
Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020, ambapo kwa mujibu wa kalenda ya NEC, kampeni zinaanza leo.
Nenda nyinyi vibaraka wa ccm
Kwanza hukai hapa
Pili wewe na Gwajima hanna tafauti
Tatu sisi kura yetu twampa Mama Mdee