NYOTA Carlos Carlinhos moja kati ya wachezaji waliopo kwenye kikosi cha wachezaji 20 watakaokwenda kuiwakilisha klabu ya Yanga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar litakaloanza kesho tarehe 5 Januari, 2020. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Mchezaji huyo rais wa Angola amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeruhi anatarajiwa kurejea kesho katika mchezo wa kwanza wa kombe hilo, ambapo Yanga watashuka dimbani kuwakabiri Jamhuri kwenye mchezo wa kundi A.
Wachezaji wengine waliokuwa katika kikosi hicho ni makipa Ramadhani Kabwili, Metacha Mnata na Farouk Shikalo, huku mabeki ni Adeyun Salehe, Paul Godfrey, Said Makapu, Kibwana Shomari na Abdallah Shaibu.

Kwenye safu ya kiungo itaongozwa na Haruna Niyonzima, Mukoko Tunombe, Zawadi Mauya, Abdikarim Yunus na Omary Chibada, huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Michael Sarpong, Yacouba Sogne, Wazir Junior, Tuisila Kisinda na Arafati Hussein kutoka timu ya vijana.
Wachezaji walioachwa kwenye kikosi hiko ni Farid Mussa, Yassin Mustafa, Deus Kaseke, Feisal Salum na Bakari Mwamnyeto ambao wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na michuano ya kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wandani (Chan)
Yanga wanatarajia kuondoka jioni ya leo 4 Januari 2020, kuelekea visiwani Zanzibar ambapo kwenye michuano hiyo wapo kundi A, sambamba na timu za Namungo na Jamhuri.
Leave a comment