Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mtoto wa Mwalimu Nyerere kuzikwa Pugu
Habari Mchanganyiko

Mtoto wa Mwalimu Nyerere kuzikwa Pugu

Marehemu Rosemary Nyerere enzi za uhai wake
Spread the love

MWILI wa Rosemary, mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere utazikwa Jumatano hii ya tarehe 6 Januari 2021, makaburi ya Kituo cha Hija, Pungu jijini Dar es Salaam. Anaripoti Brightness Boaz, Dar es Salam … (endelea) .

Rosemary alifikwa na mauti Jumamosi tarehe 01 Januari 2021 katika hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa muda mrefu.

Mtoto huyo wa mwasisi wa taifa la Tanzania na ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Bunge la Muungano, katika Bunge la tisa, aliyezaliwa mwaka 1961, enzi za uhai wake, alisema akifariki azikwe makaburi hayo ya Pugu.

Msemaji wa familia, Bkobe Nyerere alisema, Rosemary enzi za uhai wake aliomba akifariki dunia akazikwe kwenye eneo ambalo wanazikwa wafia dini ambayo hutumika kama sehemu ya hija kwa waumini wa Kikristu hususan wakatoliki.

Kwa sasa msiba uko Msasani jijini Dar es Salaam, nyumbani kwa Mwalimu Nyerere ambako watu mbalimbali wakiwemo viongozi wanakwenda kutoa salamu za pole kwa wafiwa.

Bkoke alisema, mwili wa Rosemary utawasili nyumbani hapo kesho ambapo utalala hapo na Jumatano (keshokutwa) kutakuwa na ibada ya kuaga mwili  katika Kanisa la Mtakatifu Imakulata-Upanga na baada ya kumalizika, safari ya kwenda makaburini Pugu itaanza.

Miongoni ni Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliyekwenda jana Jumapili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!