Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika
Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Dk. Bernard Konga
Spread the love

RIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, imebaini Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umepata hasara ya Sh. 156.7 bilioni, huku ikitaja sababu mbalimbali ikiwemo viongozi wa serikali wastaafu na wenza wao kupata huduma bila ya kulipia michango. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akiwasilisha ripoti hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan, leo Alhamisi, Ikulu jijini Dodoma, CAG Kichere amesema hasara hiyo imepungua kutoka kiasi cha Sh. 205.9 bilioni iliyopatikana 2021/22.

CAG Kichere wastaafu na wenza wao wanaigharimu NHIF kiasi cha Sh. 84.7 bilioni kwa mwaka.

“Changamoto nyingine inayosababisha hasara ni wastaafu kunufaika bila kuchangia, sote ni wastaafu tunaotarajiwa lakini wastaafu na wenza wa wanapata huduma bila kuchangia na hii inagharimu mfuko kiasi cha Sh. 84 bilioni kwa mwaka,” amesema CAG KIchere.

CAG Kichere amesema changamoto nyingine inayosababisha hasara ni Serikali kushindwa kuilipa NHIF fedha kiasi cha Sh. 208 bilioni ambazo inadaiwa na mfuko huo. Hata hivyo, amesema Serikali imepanga kulipa Sh. 180 bilioni mwaka ujao wa fedha wa 2024/25.

“Changamoto nyingine ni kuongezeka kwa magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza yanayogharimu mfuko kiasi cha Sh. 137.8 kwa mwaka. Hizo ndizo sababu zinazoongeza mashaka ya uhimilivu wa mfuko,” amesema CAG Kichere.

Hata hivyo, CAG Kichere amesema michango ya wanachama wa NHIF imeongezeka kwa asilimia 14.6 na matumizi yameongezeka kwa asilimia 10.

3 Comments

  • CAG KUSEMA WASTAAFU WANATIA HASARA MFUKO WA BIMA HAPO AMEKOSEA SANA! HAJUI MAANA YA BIMA. MIMI NIKIWA KAZINI NIMECHANGIA MIAKA 36 NA UKIFUATILIA MWENENDO WA MATIBABU KWA KUTUMIA BIMA YANGU NAMALIZA HATA MIAKA 3 SIJAKANYAGA HOSPITALI. SASA NIMESTAAFU YEYE ANASEMA NATIA HASARA MFUKO?? HII SIO SAWA HATA KIDOGO KUTUMIA NENO HASARA KUTIBU WASTAAFU.

  • Pamoja na hilo kuna uizi mkubwa unaendelea nadhani ndani ya shirika.Kwa mfano kuna watu wanafanya transaction za kama vile kuna huduma imetolewa na malipo yanafanywa nadhani lupitia aka until za uongo .Kila nwezi naona messages kwenye simu yangu kiasi cha sh.1 764,ooo karibu mara 4 hulipwa kwa njia hii mpaka wanaonyesha control no. na risti.Najaribu kuwapogia nhif lakini siwapati.Mimi no mstaafu na inanimate sana kuona kinachoendelea

  • Wastaafu na wenza wao,wamechangia mfuko wa NHIF kwa zaidi ya 10 kuhitimu kupata KADI ya wastaafu.Tatizo na kuchukua michango ya wanachama na kuwakopesha wafanyakazi wa NHIF kiasi kikubwa, gharama kubwa za dawa za Magonjwa yasiyo ambukizo(lakini dawa yake imeshapatikana). Serikali ilipe michango ya watumishi wa Serikali na mikopo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!