Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge lataja kinachokwamisha Mradi wa Mchuchuma na Liganga
Habari za Siasa

Bunge lataja kinachokwamisha Mradi wa Mchuchuma na Liganga

Josephat Gwajima, Mbunge wa Jimbo la Kawe (CCM)
Spread the love

 

MRADI wa uchimbaji chuma cha Liganga na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma, ulioko wilayani Ludewa, Mkoa wa Njombe, umetajwa kukwama kutokana na mwekezaji kutaka vivutio vya ziada vinavyolenga kumnufaisha kuliko maslahi ya taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 1 Februari 2023 kupitia taarifa ya shughuli zilizotekelezwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, kuanzia Februari 2022 hadi Februari 2023, iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma na mwenyekiti wake, David Kihenzile.

“Kamati ilipohoji kujua kinachokwamisha utekelezaji wa Miradi hii ilielezwa sababu au changamoto zifuatazo, mwekezaji alihitaji vivutio vya ziada vinavyolenga kumnufaisha zaidi mwekezaji kuliko maslahi ya Taifa letu. Vivutio vilivyoombwa na mwekezaji vilikuwa vikikinzana na Sheria mbalimbali nchini. Sheria hizo ni pamoja na Sheria za Kodi, Sheria ya Madini, Sheria ya Rasilimali na Maliasili za Nchi,” amesema Kihenzile akisoma taarifa hiyo.

Kihenzile amesema kuwa, kamati hiyo ilipofanya uchunguzi wake dhidi ya kukwama kwa utekelezaji wa mradi huo, ilibaiinika kuwa mkataba wa mwekezaji huyo una vipengele kadhaa vyenye mapungufu ambayo yanakinzana na maslahi ya Taifa.

“Changamoto nyingine ni kucheleweshwa na kuongezeka kwa fidia ya Wananchi kutoka Sh. 11 bilioni kwa uthamini wa mwaka 2015 hadi Sh. 15.9 bilioni mwaka 2022. Kiasi hiki kinajumuisha riba itokanayo na kucheleweshwa kwa fidia katika kipindi husika,” amesema Kihenzile.

Amesema kuwa, wakati Serikali ikijielekeza katika jitihada za kutafuta mwekezaji mwingine wa kuendeleza mradi, mwekezaji wa awali (SHG) amejitokeza tena na kudai kuwa yupo na ana uwezo wa kutekeleza mradi huo.
Mradi huo uliokwama kwa zaidi ya miaka 10, ulipangwa kutekelezwa na Kampuni ya Sichuan Hongda Group Corporation (SHG), iliyoingia ubia na Serikali Septemba 2011 kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Kihenzile amesema kamati hiyo inaitaka Serikali kuhakikisha mradi huo unaanza kutekelezwa kwa kuwa kuchelewa kwake kunachelewesha kasi ya maendeleo ya ujenzi wa viwanda mama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!