Monday , 26 February 2024
Home Habari Mchanganyiko BoT yakunjua makucha, yafunga benki tano
Habari Mchanganyiko

BoT yakunjua makucha, yafunga benki tano

Benki Kuu ya Tanzania
Spread the love

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imezifunga na kuziweka chini ya ufilisi benki tano nchini kutokana na kuwa na upungufu wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Sheria iliyovunjwa na ile ya benki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.

Uamuzi huo umetolewa leo na BoT na kwamba imefanya hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 56(1)(g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2)(i), 11(3)(c) na (j), 61(1) na 41(a) cha sheria ya benki na taasisi za fedha ya mwaka 2006.

Imezitaja benki hizo kuwa ni Covenant Bank For Women (T) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers’ Cooperative Bank Limited, na Meru Community Bank Limited.

“Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu Na. 41(a) cha sheria ya benki na taasisi za fedha ya mwaka 2006; Benki Kuu ya Tanzania imeiteua Bodi ya Bima ya Amana (The Deposit Insurance Board) kuwa mfilisi kuanzia leo tarehe 04 Januari 2018.

“Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa benki hizi zina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria.

Taarifa ya BoT imeeleza kuwa upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hizo kunahatarisha usalama wa amana za wateja wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Tembo aongoza migongano binadamu, wanyamapori

Spread the loveIMEELEZWA kuwa asilimia 80 ya migongano baina ya binadamu na...

Habari Mchanganyiko

“Watanzania tembeleeni vivutio vya utalii”

Spread the loveSHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka Watanzania kujitokeza kutembelea...

error: Content is protected !!