Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM washikana uchawi, uchaguzi wa naibu meya
Habari za Siasa

CCM washikana uchawi, uchaguzi wa naibu meya

Mussa Kafana, Naibu Meya wa Dar es Salaam. Picha ndogo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob akigombana na madiwani wa CCM kulinda kura za Naibu Meya
Spread the love

DIWANI mmoja kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), jina tunalihifadhi kwa sasa, ameibua taharuki baada ya kuamua kumpigia kura mgombea wa nafasi ya naibu meya katika halmashauri ya jiji la Dar es Salaam. Anaripoti Faki Sosi… (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya ukumbi wa mikutano wa Karimjee, jijini Dar es Salaam zinasema, diwani huyo aliamua kupigia kura mgombea wa Ukawa, Kafana Mussa Kafana, kutokana na kile kinachoitwa, “misuguano ya ndani.”

Vyama vinavyounda Ukawa, vilikuwa na wajumbe 14 katika uchaguzi huo. Lakini ni wajumbe 11 waliohudhuria mkutano huo wa uchaguzi. Wajumbe wengine watatu – Halima Mdee, Abdallah Mtulia na Leah Madibi, hawakuhudhuria mkutano huo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Mdee ameshindwa kuhudhuria mkutano huo kwa kuwa yuko nchini Afrika Kusini kwa matibabu. Naye Mtulia yuko Dodoma anakohudhuria vikao vya Kamati za Bunge; huku Leah akiwa bado hajahudhuria vikao hivyo tangu kurejeshewa uanachama wake na mahakama.

Leah ambaye ni diwani wa Viti Maalum kupitia manispaa ya Ubungo, alivuliwa unachama wake na Ibrahim Lipumba kwa madai kuwa amekisaliti chama chake. Alirejeshwa na mahakama Novemba mwaka jana akiwa pamoja na wabunge wengine wanane wa chama hicho.

Taarifa zinasema, kutokana na kutokuwapo kwa wajumbe hao watatu, vyama vya Ukawa na CCM vyote vilibaki na wajumbe halali 11 wa mkutano huo.

Hata hivyo, Ukawa ililazimika kutimiza idadi hiyo baada ya kumleta diwani wake wa Kiwalani (CUF), ambaye ndiye aliyekuwa anawania nafasi hiyo kwa machela kutokana na kuwa mgonjwa.

Ukawa ni muunganiko vyama vinne vya siasa – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), CUF, NCCR-Mageuzi na National League Democrat (NLD).

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliotawaliwa na ubabe, mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana alisema, jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa ni 22.

Alisema, mgombe wa CCM, Mariam Lulida amepata kura 10 na Kafana amepata kura 12 na kwamba kwa matokeo hayo, “Kafana Mussa Kafana, ndiye mshindi halali wa uchaguzi huu.”

Mara baada ya kutangaza matokeo hayo, ukumbi wa Karimjee kulilipuka kwa shagwe huku mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea akiwa amebebwa juu na wafuasi na viongozi wa vyama kutokana na kazi kubwa aliyokuwa ameifanya kuhakikisha ushindi unapatikana.

“Tunakupongeza sana mheshimiwa Kubenea. Tunakupongeza sana ndugu yetu, kwa kazi hii kubwa mlioifanya. Tunakushukuru kwa kulikomalia jambo hili hadi mwisho,” alieleza Mustafa Muro, diwani kutoka manispaa ya Kinondoni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!