Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara BoT: Akiba fedha za kigeni inaweza kuagiza bidhaa miezi minne
Biashara

BoT: Akiba fedha za kigeni inaweza kuagiza bidhaa miezi minne

Spread the love

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imewatoa hofu Watanzania kuhusu uhaba wa fedha za kigeni hususani Dola za Marekani na kubainisha kuwa mbali na dunia kukumbwa na changamoto za kiuchumi zinazosababisha uhaba wa fedha hizo kwa upande wa Tanzania hali ni shwari kwani inayoakiba ya kutosha kuagiza bidhaa na huduma kwa zaidi ya miezi minne. Anaripoti Gabriel Mushi…(endelea).

Hayo yamebainishwa leo Jumanne jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dk. Suleiman Misango wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu uhaba wa dola za Marekani duniani.

Amesema BoT inayo akiba ya Dola za Marekani bilioni 4.9 ambazo zinatosha kuagizaji wa bidhaa na huduma kwa zaidi ya miezi minne.

Ameongeza kuwa licha ya kuwepo kwa uhaba huo, BoT kila siku wanauza Dola za Marekani milioni mbili katika Soko la fedha za kigeni kati yake na mabenki (IFEM).

Ameongeza kuwa vita ya Ukraine ilipoanza walikuwa wanauza dola 500,000 kwa siku lakini kadiri ziku zinavyosonga mbele wameongeza hadi milioni mbili katika Soko la fedha za kigeni kati yake na mabenki (IFEM).

“Kuanzia mwezi Januari hadi Mei mwaka huu BoT imeuza dola za Marekani 376 milioni katika Soko la fedha za kigeni kati yake na mabenki (IFEM),” Dk. Misango.

Aidha, alisema kuwa kati ya Julai hadi Septemba ni kipindi kizuri cha kufanya biashara ya utalii ambapo fedha za kigeni zitamiminika kwa wingi hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kuhu hali ya fedha za kiugeni ingawa wasishawishike kutumia hovyo fedha hizo za kigeni.

“Ukilinganisha na nchi nyingine tunazolingana nazo kiuchumi sisi tupo vizuri katika akiba ya fedha za kigeni, hatua tunazochukua ni kujilinda ili kuwa vizuri hata ikiwa hali ya hatari itaendelea kama hivi katika soko la dunia,” alisema.

Alifafanua kuwa mtikisiko huo wa uhaba wa fedha za kigeni hususani dola za Marekani umesababishwa na janga la maambukizi ya ugonjwa wa Uviko 19, mabadiliko ya tabia nchi na vita kati ya nchi za Urusi na Ukraine ambavyo vinaendelea hadi sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cash Days Promo mamilioni yanakusubiri, cheza kupitia Meridianbet kasino 

Spread the love  JIANDAE kwa mshangao wa kustaajabisha Meridianbet kasino ya mtandaoni...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!