BODI ya Mamlaka ya Ngorongoro (NCAA), imesema itakabiliana na changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo kufikia dira ya uhifadhi, anaandika Mwandishi Wetu.
Kaimu Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Mudhihir Mudhihir, amesema hayo juzi baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kuizindua jijini hapa.
Amesema wajumbe wa bodi hiyo ambao ni wabobezi wa taaluma mbalimbali na uzoefu wataweza kuisimimia mamlaka hiyo kufikia azma yake.
“Kila mmoja wetu hapa ana taaluma aliyobobea nayo, kwa mfano, tunao wataalam wa IT, wastaafu wa jeshi na wanasiasa…na muunganiko huo utaweza kuleta matunda mazuri kwa mamlaka,” amesema.
Wajumbe wa bodi mpya, imechukua nafasi ya bodi ya zamani ambayo muda wake ulimalizika Mei mwaka huu.
Wajumbe wa bodi ya sasa ni Simon Sayore, Brigadia Jenerali mstaafu Aloyce Mwanjile, Dk. Aikande Kwayu, Godfrey Leyla na Mhandisi Peter Ulanga.
Wengine ni Profesa Audax Mabula, Dk Fred Manongi, Profesa Kalunde Sibuga na mbunge wa zamani wa Namtumbo, Vita Kawawa.
Leave a comment