August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakili Makene alilia fedha za ada ya TLS

Nyundo ya Hakimu

Spread the love

WAKILI wa kujitegemea ambaye pia ni mwanachama wa Chama Cha Mawakili Tanzania Bara(TLS), Emmanuel Makene amekilalamikia Chama hicho kuwa hakiwasaidii wanachama wake wakati wanatoa ada kila mwaka, anaandika Jovina Patrick.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Makene, amesema kila mwaka mwanachama analipa zaidi ya Tsh. 2,000,000 kwenye chama cha Mawakili lakini pesa hizo haziwasaidii kwa chochote kwani hata wakipata tatizo hakuna msaada wowote kutoka katika chama hicho.

“Wawakili tunatumia zaidi ya 2,000,000 hadi 4, 000,000 kwa mwaka kwa kulipa kwenye chama cha mawakili,” anasema Makene.

Amesesma kuwa kwa mawakili wapya hali hiyo inawawia vigumu kwani kabla msomi huyo hajasajiliwa anatakiwa kulipa pesa kwenye chama bila hivyo hawezi kupewa usajili.

“Kwa mawakili wapya kabla mtu hajasajiriwa kuwa wakili anapaswa alipe hela kwenye chama. Sasa kwa mtu anayemaliza chuo anapata wapi hela za kulipa?” anahoji Makene.

error: Content is protected !!