Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bendera ya NMB yasimikwa Mlima Kilimanjaro
Habari Mchanganyiko

Bendera ya NMB yasimikwa Mlima Kilimanjaro

Spread the love

WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB nchini Tanzania wamefanikiwa kupanda na kusimika bendera ya taasisi hiyo kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro kama sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Benki hiyo pia imelitumia tukio hilo kama sehemu ya kuwahamasisha wafanyakazi wake na Watanzania kwa ujumla kushiriki utalii wa ndani ili kusaidia kukua kwa shughuli hiyo yenye fursa lukuki kibiashara na tija kiuchumi.

Wafanyakazi wa benki ya NMB wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutunikiwa vyeti waliporejea baada ya kupanda na kuushuka mlima Kilimanjaro katika kusherekea huduma kwa wateja kwa Benki hiyo. Wafanyakazi hao walitumia siku saba kupanda na kuushuka mlima na kuisimika bendera ya Benki ya NMB kileleni mwa Mlima huo mrefu zaidi Afrika.

NMB imeanza rasmi kushiriki kuutangaza utalii wa ndani hivi karibuni na kutangaza kushiriki kusaidia kuchangia kukua kwake Jumamosi iliyopita huko Moshi wakati wa kuwapokea wafanyakazi wake sita waliofanikiwa kupanda mlima huo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye lango la Mweka, Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Benki ya NMB, Dismas Prosper alisema timu ya watu sita iliyokwea mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika ilitumia siku saba.

Alisema kufanikiwa kwa timu hiyo kusimika bendera ya NMB kwenye kilele cha Uhuru ni jambo kubwa kwa wafanyakazi hao na benki hiyo ambayo ndiyo kinara katika shughuli na huduna za kifedha nchini.
“Kwanza kabisa, dhamira ya safari hii ni kufanikiwa kuupanda Mlima Kilimanjaro na kusimika bendera ya Benki ya NMB kwenye kilele chake kama namna ya kipekee kwetu kusherekea Wiki ya Huduma kwa Wateja,” alisema Prosper.

Wafanya kazi wa Benki ya NMB wakiwa katika kilele cha mlima Kilimanjaro nma bendera ya Benki hiyo kama ishara ya kusherekea huduma na kuzifikisha juu ya mlima huo. Wafanyakazi hao walitumia siku saba kupanda na kuushuka mlima na kuisimika bendera ya Benki ya NMB kileleni mwa Mlima huo mrefu zaidi Afrika.

“Pia uongozi wa NMB unalitumia zoezi ili la kuupanda Mlima Kilimanjaro kuhamasisha utalii wa ndani na kuchangia maendeleo ya shughuli za kitalii nchini,” kiongozi huyo alisema.
Prosper alisema tukio la kusherekea Wiki ya Huduma kwa Wateja mita 5,895 juu ya usawa wa bahari kuna maana kubwa kwa namna benki hiyo inavyozingatia huduma bora kwa wateja na katika nafasi yake kama kiongozi wa kibenki sokoni.

Aidha, ni kitendo cha kutambua umuhimu wa biashara wa utalii na jukumu la msingi sekta hiyo katika uchumi wa taifa na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Naye Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro, Iman Kikoti, alisema kitendo cha wafanyakazi wa NMB kupanda Mlima Kilimanjaro kinaimarisha nafasi ya benki hiyo kuendelea kuwa karibu na sekta ya utalii na mshirika wa kimkakati wa maendeleo ya taifa.

Pia alibainisha kuwa uamuzi wa NMB wa kuhamasisha utalii wa ndani ni kielekezo cha utayari wake kuchangia maendeleo na ustawi wa tasnia hiyo ili iweze kuchangia kikamilifu kuchochea kukua kwa uchumi nchini na ujenzi wa taifa.

Kikoti alipongeza NMB kwa hilo alisema utalii wa ndani ni hazina kubwa kwa taifa ambayo inahitaji ushirikiano wa wadau kuufanya kushamili na kuchangia kukua kwa sekta nzima ya utalii nchini.
“Kwa sasa mchango wa utalii bado ni mdogo kwa hiyo uamuzi wa NMB kusaidia kuuchangamsha ni jambo jema na la kimaendeleo linalopaswa kuungwa mkono na wadau wote wa sekta binafsi,” alibainisha.

Kiongozi wa safari hiyo iliyoanza tarehe 8 Oktoba kwenye Lango la Machame, Alfred Shayo ambae pia ni Afisa mkuu wa wateja wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, alisema kamwe hawatajutia kushiriki kwenye zoezi hilo lilowafunza mambo mengi ya kimaisha na kikazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!