HIFADHI ya Taifa ya Serengeti imeshinda tuzo ya Hifadhi bora zaidi barani Afrika 2022 ikiwa ni mara ya nne mfululizo baada ya kushinda tena mwaka 2019, 2020 na 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Hifadhi hiyo imezibwaga hifadhi za Central Kalahari ya Botswana, Kruger National Park ya Afrika Kusini, Kidepo Valley Nationa Park (Uganda), Etosha National park (Namibia) na Masai Mara National Reserve ya Kenya.
Tuzo hizo zilizoanzishwa mwaka 1993 kutambua na kutunza ubora wa urithi huo wa rasilimali za hifadhi, zinatolewa World Travel Award (WTA) na zinatambulika kimataifa.
Serengeti ni miongoni mwa hifadhi 19 zilizopo chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambazo zimetapakaa katika kanda za Kusini, Kaskazini, Mashariki na Magharibi.
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyopo mkoani Mara ipo kanda ya Kaskazini ikiwa maarufu kwa tukio la kipekee la kuhama kwa mamilioni ya nyumbu ambayo huvuka mto Mara kila mwaka.
Leave a comment