Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari Beki wa zamani wa Yanga, Taifa Stars afariki Dunia, kuzikwa kesho
HabariMichezo

Beki wa zamani wa Yanga, Taifa Stars afariki Dunia, kuzikwa kesho

Spread the love

 

MLINZI wa zamani wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Ally Mtoni maarufu kama Sonso amefariki Dunia hii leo mchana, kwenye Hospital ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kugua katika kipindi cha muda mfupi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Klabu ya Yanga kupitia kurasa mbalimbali za mitandao yao ya kijamii, walithibitisha taarifa ya kifo cha mlinzi wao huyo wa zamani, ambaye mapaka umauti unamkuta alikuwa akicheza kwenye klabu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani.

Katika taarifa ya klabu hiyo ilieleza kuwa kifo cha mchezaji huyo wao wa zamani na Taifa Stars, kilitokea kwenye Hospital ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa kutoka kwa ndugu wa mchezaji huyo zimeeleza kuwa mazishi yatafanyika siku ya kesho tarehe 12 Februari 2022, majira ya saa 10 jioni kwenye makaburi ya Magomeni jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe Sonso alikuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 30, walioshiriki michuano ya kombe la Mataifa Afrika 20219 nchini Misri chini ya kocha Emmanuel Amunike raia wa Nigeria

Katika enzi za uhai wake Sonso amewahi kutumikia klabu za Kmc ilivyokuwa Ligi daraja la kwanza, Lipuli FC, Yanga, Kagera Sugar na Ruvu Shooting.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!