Spread the love

 

BEKI wa kati wa klabu ya Yanga, Dikson Job amefungiwa michezo mitatu na kupigwa faini ya shilingi 500,000 kufuatia kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Mbeya City Richardson Ng’odya kwenye mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara ulizokutanisha timu hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Adhabu hiyo imetolewa leo tarehe 11 Februari 2022, kupitia kamati ya uwendeshaji na usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72),katika kikao chake kilichokaa Februari 10 mwaka huu kupitia matukio mbalimbali na mwenendo wa Ligi hiyo.

Job anakuwa mchezaji wa pili wa klabu ya Yanga kufungiwa kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22, mara baada ya siku chache za nyuma kamati hiyo kumfungia michezo mitatu beki wa kulia wa klabu hiyo Raia wa Jamhuri ya Congo Djuma Shabani.

Djuma ambaye kwa sasa amebakiksha mchezo mmmoja kumaliza adhabu yake na kwenye mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara atarejea dimbani.

Maamuzi ya kamati hiyo pia yaliwagusa moja kwa moja klabu ya Yanga, kufuatiwa kutozwa faini ya shilingi 1,000,000 kufuatia mashabiki wa klabu hiyo kuwapiga na makopo waamuzi waliokuwa wanachezesha mchezo kati yao na Mbeya City ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Licha ya kupewa adhabu hiyo sambamba na onyo kali kufuatia kuwaonesha vitendo visivyo vya kuungwana, waamuiz wawili Hussen Athuma kutoka Katavi ambaye alikuwa mwamuzi wa kati na Geofrey Msakila ambaye alikuwa mwamuzi namba mbili kutoka Geita wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu kwa mizunguko mitatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *