Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Basi la Magereza lagonga treni yenye abiria 650 Dar
Habari MchanganyikoTangulizi

Basi la Magereza lagonga treni yenye abiria 650 Dar

Spread the love

Basi  Jeshi la Magereza lenye namba MT 0040 limegonga treni ya abiria namba YD16 yenye injini namba 9015 iliyokuwa ikitokea mikoa ya Bara (Morogoro, Dodoma, Tabora na Kigoma) katika eneo la Ukonga jjini Dar es Salaam, muda wa saa 11:25 leo Ijumaa  jioni. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Basi hilo la Magereza lililokuwa limebeba watu 15 liliigonga na treni namba YD16 yenye injini namba 9015 iliyobeba abiria 650 wakati basi hilo likivuka reli eneo la Kilomita 13 (Ukonga Magereza).

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano kutoka Shirika la Reli Tanzania, Jamila Mbarou imesema ajali hiyi imesababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 10 ambao kati yak wanawake watano na wanaume watano.

Amesema majeruhi wamewahishwa katika Hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu.

“Shirika linaendelea kuwasihi madereva wa vyombo vya moto kuwa makini wanapokatiza reli kufuata Sheria na alama za usalama wa reli zilizowekwa ili kuepusha ajali.

“Shirika linatoa pole kwa ndugu wa marehemu na Mwenyezi Mungu awape nafuu majeruhi ili waweze kuendelea na shughuli za kujenga Taifa, taarifa zaidi zitaendelea kutolewa,” amesema.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

error: Content is protected !!