WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla kusimamia usitishwaji wa zuio la bodaboda na bajaji kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Bashungwa amechukua hatua hiyo kufuatia uamuzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam la kupiga marufuku bodaboda na bajaji kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam isipikuwa maeneo yakiyoainishwa.
Katika taarifa iliyotolewa na Tamisemi leo tarehe 21 Aprili, 2022 imesema bila shaka nia kusitisha vyombo hivyo vya usafiri ilikuwa ni njema, ila dosari ipo kwenye namna ya kushughulikia jambo lenyewe.
“Bila shaka nia ni njema, ila dosari ipo kwenye handling (kushughulikia) ya jambo lenyewe. Serikali yetu ya Awamu ya Sita inatambua na kuthamini ajira za vijana wetu za bodaboda na bajaji kuwa ni ajira rasmi na wanajipatia riziki na familia zao.
“Namuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Amos Makalla kusimamia usitishwaji wa zuio hilo ili kutoa nafasi ya kufanya tafakuri zaidi,” imesema tyaarifa.
Tangazo la kusitisha vyombo hivyo vya usafiri kuingia katikati ya Jiji lilitolewa tarehe jana tarehe 20 Aprili 2022.
Wewe waziri umeona jinsi boda boda wanavyoendesha ? Ni hatari kwa maisha! Hawaheshimu sheria hata asilimia moja!!
NI VURUGU TUPU