Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Bandari za Tanga na Mtwara hazihusiki uwekezaji DP World
BiasharaTangulizi

Bandari za Tanga na Mtwara hazihusiki uwekezaji DP World

Spread the love

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesisitiza kwamba uwekezaji wa kampuni ya DP World kutoka Dubai hautahusisha bandari zote nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea.)

Amesema kwamba katika Awamu ya Pili ya Mkataba huo, chombo kitakachokuwa na mamlaka ya kuchagua bandari zinazoweza kuhusika katika uwezekezaji huo katika bandari za Bahari na Maziwa, ni Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Aidha amesema uwekezaji huo hautahusisha Bandari ya Tanga na Mtwara kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakizusha.

Akiwasilisha bungeni maelezo ya awali kuhusu mapendekezo ya kuridhia mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai katika ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari za Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine

Mikataba Mahsusi ya Miradi (Project Agreements) itajadiliwa na kuingiwa kwa kila eneo la ushirikiano na itahusisha matumizi ya ardhi pekee na sio umiliki wa ardhi.

“Msisitizo wa Serikali ni kuhakikisha maeneo yote ya nchi yanabaki chini ya umiliki wa Serikali” amesema Mbarawa.

Aidha, amesema taasisi zote za Serikali ambazo zinahusika katika shughuli za bandarini zitaendelea kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria ndani ya eneo la bandari.

“Uwepo wa sekta binafsi kutoa huduma katika maeneo ya bandari umeendelea kuwepo na kusimamiwa na Serikali kwa miongo tofauti tofauti. Aidha, katika kipindi chote ambacho Sekta Binafsi imehusishwa katika uendeshaji wa bandari. Hakujawahi kujitokeza tukio la kuhatarisha usalama wa nchi,” amesema.

Ameongeza kwamba “Mawanda ya uwekezaji chini ya Mkataba huu yatahusisha uendelezaji na uendeshaji wa baadhi ya maeneo ya Bandari na sio bandari yote kwa ujumla wake.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cash Days Promo mamilioni yanakusubiri, cheza kupitia Meridianbet kasino 

Spread the love  JIANDAE kwa mshangao wa kustaajabisha Meridianbet kasino ya mtandaoni...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

error: Content is protected !!