WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa leo Jumamosi amewasilisha bungeni maelezo ya awali kuhusu mapendekezo ya kuridhia mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai katika ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari za Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa hali ya sasa ya utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam imeendelea kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na bandari shindani kikanda. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Amesema Serikali imeendelea kuwekeza kwenye bandari zake kwa vipindi tofauti kwa kutumia vyanzo vyake na fedha za mikopo katika kutekeleza mikakati kwa lengo la kuboresha sekta ya bandari nchini.
“Pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, bado ufanisi katika utoaji huduma za bandari haujafikia viwango vinavyotakiwa kimataifa.
“Kwa mfano, gharama ya kusafirisha kasha moja kutoka nje ya nchi (on transit) kwenda nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zinafikia takriban Dola za Marekani kati ya 8,500 hadi 12,000. Hii ni gharama kubwa sana ikilinganishwa na Bandari shindani,” amesema.
Leave a comment