May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam FC waitaka Simba nusu fainali

Spread the love

 

MARA baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, dhidi ya Rhino Rangers kocha msaidizi wa Azam FC vivie Bahati anaitaka klabu ya Simba kwenye nusu fainali kwa kuwa anaamini itakuwa mchezo mzuri. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa robo fainali ya tatu wa michuano ya kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation) ulichezwa kwenye Uwanja wa Ccm Kambarage mkoani Shinyanga na kuifanya Azam kutangulia kwenye nusu fainali huku akisubili mshindi kati ya Simba na Dodoma Jiji FC utakaochezwa muda mfupi ujao.

Mara baada ya mchezo huo kukamilika kocha msaidizi wa Azam FC Vivie Bahati aliwaombea Simba kushinda mchezo wa hapo baadae ili wakutane kwenye nusu fainali na kuamini kuwa utakuwa mchezo mzuri.

“Ili mechi iwe nzuri tunataka Simba ipite utakuwa mchezo mzuri sana kwenye michuano hii.” Alisema Vivie Bahati

Vivie Bahati, kocha msaidizi wa Azam FC

Simba itashuka dimbani muda muchache kumenyana na Dodoma Jiji FC kwenye robo fainali ya nne ya michuano hiyo katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kwenye mchezo huo Rhino walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Abdallah … kwenye dakika ya 32 na dakika mbili baadae Azam FC walifanikiwa kuchomoa kupitia kwa Ayoub Lyanga kwenye dakika ya 34 na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko wakiwa wamefunga bao 1-1.

Kipindi cha pili kilirejea na Azam FC walifanikiwa kupata bao la pili kwa njia ya mkwaju wa penati lililofungwa na Agrey Morris kwenye dakika ya 65 na baadae Obrey Chirwa aliyeingia kuchukua nafasi ya Prince Dube akakamilisha mchezo huo kwa kupachika bao la tatu kwenye dakika ya 81.

Mohammed Hussein, mchezaji wa Simba

Kwa matokeo hayo Azam FC anakamilisha idadi ya timu tatu zilizotinga hatua ya usu fainali ambapo ni Yanga na Biashara United.

 

error: Content is protected !!