Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Bajeti ya ardhi 2021/22 yapungua kwa 64.2%
Habari Mchanganyiko

Bajeti ya ardhi 2021/22 yapungua kwa 64.2%

Spread the love

 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, imesema bajeti ya maendeleo katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022, imepungua kwa asilimia 64.2. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Kamati hiyo imetoa taarifa hiyo leo tarehe 26 Mei 2021, ikiwasilisha maoni yake kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, kwa mwaka ujao wa fedha, kuwasilishwa bungeni.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamati hiyo, bajeti ya maendeleo ya wizara ya ardhi imepungua kutokana na kukosekana kwa fedha za miradi ya maendeleo, kutoka nje.

“Punguzo la bajeti ya mpango wa maendeleo kwa mwaka wa fedha 2021/2022, limesababishwa na kukosekana kwa fedha za miradi ya maendeleo, kutoka nje kwa asilimia 100,” imesema taarifa hiyo.

Kamati hiyo imeishauri wizara kutafuta wadau wa maendeleo, badala ya kutegemea fedha za nje.

“Wizara imetakiwa kujikita na kuzingatia ushauri wa kamati, wa kutenga fedha zaidi za ndani , kuliko za nje katika kukamilisha miradi iliyopo,”

“Hata hivyo, ni maoni ya kamati kwamba, Serikali iendelee kutafuta wadau wa maendeleo ili kuchochea mahusiano na kusaidia kufikia lengo la kibajeti. Iendelee kutafuta ahadi zote za fedha za nje, ili ziweze kuziba pengo la kibajeti,” imesema taarifa hiyo.

Bunge la Tanzania

Taarifa ya kamati hiyo imesema, fedha za bajeti hiyo zimepungua kutoka Sh. 84.08 bilioni, zilizoidhinishwa na bunge 2020/2021, hadi kufikia Sh. 29.55 bilioni, ambazo wizara hiyo imeliomba Bunge liidhinishe katika 2021/2022.

“Katika mwaka wa fedha 2021/2022, wizara inaomba kuidhinishiwa Sh. 29.55 bilioni , kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ukilinganisha na Sh. 84.08 bilioni, zilizoidihinishwa mwaka wa fedha 2020/2021,” imesema taarifa ya kamati hiyo.

Taarifa hiyo imesema “hii ni sawa na pungufu la asilimia 64.2. Kati ya fedha inayoombwa, Sh. 18.30 bilioni, ni fedha za ndani ukilinganisha na Sh. 17.78 bilioni, zilizoidhinishwa katika mwaka wa fedha unaoisha.”

“Na Sh. 11.25 bilioni ni fedha za nje, ukilinganisha na Sh. 66.30 bilioni, zilizoidhinishwa katika Mwaka wa fedha unaoisha,” imesema kamati hiyo.

Kati ya fedha hizo, Sh. 47.40 bilioni, ilitengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh. 84. 08 bilioni, kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Katika bajeti ya maendeleo, shilingi bilioni 17,787,522,032 zilikuwa ni fedha za ndani na shilingi bilioni 66,300,839,000 ni fedha za nje.

Kati ya fedha zilizopokelewa, shilingi bilioni 39,266,711,047 ni kwa ajili ya Matumizi ya kawaida sawa na asilimia 76.65 ya bajeti iliyotengwa kwa shughuli hiyo na shilingi bilioni 5,375,695,164 sawa na 30.2% zilikuwa ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Katika Bajeti ya Maendeleo iliyopokelewa, shilingi bilioni 5,375,695,164 sawa na 30.2% zilikuwa ni fedha za ndani. Aidha, shilingi bilioni 66,300,839,000 ambazo zilikuwa ni fedha za nje na hazikupokelewa kabisa. Jedwali lifuatalo linaonesha mwenendo wa upatikanaji wa fedha wa Fungu 48 kwa Mwaka 2020/2021.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2020/2021, Fungu 03 – Tume ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi iliidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 4,664,768,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Hadi kufikia tarehe 15 Machi, 2021 Tume ilipokea jumla ya shilingi bilioni2,011,950,150 sawa na 43% ya fedha iliyoidhinishwa.

Kwa upande wa bajeti ya maendeleo, Tume iliidhinishiwa shilingi bilioni 1,500,000,000 na hadi kufikia tarehe 15 Machi, 2021 Tume ilikuwa bado haijapokeafedha za maendeleo kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa miradi yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!