Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Tangulizi Chadema yabadili upepo, Mbowe ataja mikakati mipya
Tangulizi

Chadema yabadili upepo, Mbowe ataja mikakati mipya

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeamua kuachana na siasa za kiharakati, badala yake kinakuja na siasa shirikishi. Anaripoti Nasra Bakari, DMC…(endelea ).

Taarifa hiyo imetolewa jana tarehe 27 Mei 2021 na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, akizungumza katika Baraza la Mashauriano la chama hicho, Mkoa wa Arusha.

Mbowe alisema, Chadema kimeamua kulegeza kidogo siasa zake, ili zisiwe za mitulinga, na kuagiza viongozi na wanachama wake, kutengeneza miakakati shirikishi, itakayokitambulisha chama hicho kwa Watanzania.
“Leo (jana) ndugu zangu tukarudi tena kwenye kikao kurekebisha yale tuliyopanga ya siasa za mitulinga, tukakubaliana tulegeze kidogo siasa zetu zisiwe za mitulinga,” alisema Mbowe.

Mbowe alisema “tukatengeneze mikakati shirikishi ambayo itakitambulisha chama chetu, kama tumaini pekee kwa Watanzania wote waliopitia maumivu na mateso makubwa, kwa kipindi cha miaka mitano.”

Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema, chama hicho kimemua kufanya operesheni itakayofahamika kwa jina la ‘Operesheni Haki’, itakayofanyika katika kanda 10 za chama hicho, kwa ajili ya kudai masuala mbalimbali kuhusu uimarishwaji shughuli za kisiasa nchini.

“Tunajua chama chetu kina kanda 10, mbili visiwani Zanzibar, nane Tanzania Bara, tukatengeneze na kubuni mikakati makini ya chama, inayoweza kuchambua changamoto mbalimbali inazokabili viongozi na wanachama,”

“Tumepanga ratiba ya mwezi mmoja na nusu ya kufanya jambo hili (Operesheni haki) na tunasema hili jambo tulifanye kwa uhakika, tusiende kila mahali ila tuchague maeneo maalum kwa sababu maalum,” alisema Mbowe.

Mbowe alisema, Chadema kitahakikisha kinatumia operesheni hiyo, kupata suluhu ya changamoto mbalimbali zilizojitokeza nchini, ikiwemo katika chaguzi, demokrasia na uhuru wa vyama vya siasa katika kutekeleza majukumu yake.

“katika operesheni hiyo, haya mawazo tuliyokuwa nayo tukayageuze kuwa vitendo hadi turidhike kwamba jambo hili limepokelewa, linatekelezeka na linastahili kuendelezwa,” alisema Mbowe.

Pia, Mbowe alisema, dhumuni la operesheni hiyo ni kukishusha chama hicho kwa wananchi.

“Operesheni tunayoiita operesheni haki, au kwa lugha ya kiingereza tunaiita grass rout , Kiswahili chake ni ngazi ya chini kule kwenye mizizi yetu ya chama. Chama hiki tukitoe kule juu Taifa, tuwashushie wananchi chama chao, wakaksimamie, wakijenge kule kwenye makazi yao,” alisema Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

error: Content is protected !!